DHANA YA AFYA MOJA YAANZA KUTEKELEZWA KWA VITENDO MPAKANI NAMANGA


Na.  OWM, Namanga.
Tanzania kwa kushirikiana na Kenya  tarehe 11 Juni, 2019, wameanza kutekeleza zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, lilofunguliwa jana mpakani mwa Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga, ambalo linatekelezwa kwa siku nne,  kuanzia tarehe 11 hadi 14 Juni mwaka huu.


Zoezi hilo, linazingatia Dhana ya Afya moja ambayo hujumuisha sekta ya afya ya binadamu, wanyamapori, mifugo na mazingira katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu. Wataalamu wa sekta hizo  tarehe 12, Juni, 2019, wameendelea kutekeleza  zoezi hilo kwa kuzingatia Dhana hiyo.

Wataalamu wa sekta za Afya wa Tanzanaia na Kenya, katika makundi tofauti wameweza kutekeleza kwa vitendo kwa kutumia Dhana ya Afya moja katika  kuhakiki matumizi ya maabara zinazohamishika, kutathmini uwezo wa uchunguzi na usimamizi wa wagonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa mpakani, pamoja na kufanyia majaribio ya utekelezaji wa Mipango ya Dharura ya Taifa na Kanda, Miongozo ya Utendaji katika kukabili na kupunguza madhara ya Bonde la  Homa ya Ufa kwa Wanyama na Binadamu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527