CHIRWA NA WENGINE 7 WAPIGWA PANGA AZAM FC

Klabu ya Azam FC imetangaza kuachana na Nyota wake 8 ambao inaelezwa kuwa mikataba yao imemalizika hivyo hawataongeza na kuanzia sasa ni wachezaji huru.


Afisa Habari wa Klabu hiyo Jaffar Idd Maganga amesema kuwa uongozi wa juu tayari umeshafanya mazungumzo na wachezaji hao na umewapa ruhusa ya kuangalia timu nyingine.

Maganga  amewataja wachezaji hao kuwa ni nyota wa zamani wa Yanga Obrey chirwa, nyota wa zamani wa Simba Daniel Lyanga na Ramadhani Singano. 

Wengine ni Joseph Kimwaga, Enock Atta, Tafadzwa Kutinyu, Steven Kingue na Hassan Mwasapili.

Maganga amesema kuwa Azam FC inawashukuru wachezaji hao, kwa mchango wao mkubwa walioutoa ndani ya Klabu hiyo na wana imani watafanya vizuri huko waendako.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527