ALICHOKISEMA GODBLESS LEMA KUHUSU KAULI YA RAIS MAGUFULI 'KUWAACHA MABILIONEA 100'


Jana Rais John Magufuli alitoa kauli ya kwamba anatamani atakapomaliza muda wake wa uongozi aache mabilionea 100 nchini Tanzania kauli ambayo imemuibua Mwanasiasa wa Upinzani, Godbless Lema.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka Wilaya zote nchini kwenye mkutano wa siku nzima uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.

Kauli hiyo ya Magufuli imeonekana kuwakuna baadhi ya wanasiasa, akiwemo mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ambaye alitumia mtandao wa kijamii wa Twitter kueleza  hisia zake kutokana na kauli hiyo ya Magufuli.

Lema alieleza kuwa hotuba ya Rais Magufuli katika mkutano huo imejaa matumaini hasa kwa kauli yake ya kuacha mabilionea 100.

“Kauli ya Rais kuwa anataka kuona Tz ya mabilionea100 kabla ya utawala wake ni kauli ya matumaini kwa Nchi.Kauli hii ina thamani kubwa kuliko ile ya matajiri kuishi kama mashetani.

"Nimemsikiliza Rais naona kama anasisitiza uwepo wa utawala bora/sheria ktk ngazi zote za Serikali..”



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527