WAZIRI MKUU TERESA MAY ATANGAZA KUJIUZULU

Theresa May kujiuzulu kama kiongozi wa chama cha Conservative tarehe 7 Juni na kutoa fursa kuidhinishwa mchakato wa kuchaguliwa waziri mkuu mpya Uingereza.

Katika taarifa iliyojaa hisia aliyoitoa huko Downing Street, Bi May amesema amefanya "kila awezalo" kutekeleza matokeo ya kura ya maoni kuhusu EU ya mnamo 2016.

Ni jambo linalosalia kuwa "na majuto mengi" kwamba ameshindwa kutimiza Brexit - Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, ameongeza.

Lakini waziri mkuu mpya ndio suluhu " kwa manufaa ya taifa".

Bi May amesema ataendelea kuhudumu kama waziri mkuu wakati kukitarajiwa kuidhinishwa mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa chama cha Conservative.

Atajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho Juni 7 na uteuzi wa waziri mkuu mpya unatarajiwa kuanza wiki inayoafuata baada ya hatua hiyo.
Theresa May Uongozini

Miaka 3 ahudumu kama waziri baada ya kuondoka David Cameron

Miaka 6 kabla ya hapo, waziri wa mambo ya ndani

Ashindwa katika uchaguzi mkuu 2017 , lakini alisalia waziri mkuu

Asaliampiga kura katika kura ya maoni ya EU mnamo 2016

Brexit iligubika muda aliohudumu 10 Downing Street BBC

Sauti yake ilittereka na alikuwa mwingi wa hisia alipomaliza hotuba yake akisema: "Nitaondoka katika wadhifa huu hivi karibuni lakini imekuwa heshima kubwa maihsani mwangu kuhudumu.

"Waziri mkuu mwanamke wa pili, na bila shaka sio wa mwisho.

"Nachukua hatua hii bila ya uovu wowote, bali na shukrani za dhati na kubwa kutokana na kupata fursa kuitumikia nchi ninayoipenda."
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post