WAZIRI LUGOLA AWA MBOGO KWA POLISI WALIOWAFANYIA VURUGU WAWEKEZAJI KIWANDA CHA TUMBAKU MOROGORO | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, May 19, 2019

WAZIRI LUGOLA AWA MBOGO KWA POLISI WALIOWAFANYIA VURUGU WAWEKEZAJI KIWANDA CHA TUMBAKU MOROGORO

  Malunde       Sunday, May 19, 2019
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, amesema hatamvumilia askari au mtumishi aliyeopo chini ya wizara hiyo iwapo atabainika anamnyanyasa, kumtishia au kumsumbua mwekezaji anayefuata sheria  ikiwamo kulipa kodi.


Lugola amesema hayo jana mjini Morogoro alipozungumza na viongozi wa Kampuni ya Tumbaku ya Tanzania Leaf.

Amesema askari atakayebainika kufanya hivyo sheria dhidi yake itachukua mkondo wake kwani kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wawekezaji kuonewa na baadhi ya vyombo vya ulinzi bila sababu, huku wakitishiwa na kuapa kuwa atakayebainika atamfukuza kazi mara moja.

Pia, amesema hivi karibuni uongozi wa kampuni hiyo uliwasilisha malalamiko kwa ofisi ya Waziri Mkuu kutokana na viongozi wake wakuu kunyanyaswa na kutishiwa kukamatwa na polisi mkoani Morogoro.

Lugola amesema Serikali imedhamiria kufikia uchumi wa kati kwa sekta ya viwanda na kwamba, imetoa nafasi kubwa kwa wawekezaji kuwekeza nchini kwa kufuata sheria zilizopo.

“Lakini kumekuwapo na baadhi ya watumishi ndani ya wizara hii wakiwamo baadhi ya askari kuwabugudhi kwa kutaka kujipatia kipato, sasa niwaonya acheni tabia hiyo,” ameonya Lugola.

Pia, Lugola ameagiza uongozi wa Polisi Mkoa wa Morogoro kumpa taarifa za kina ili kuwachukua hatua kwa waliofanya vitendo hivyo ili wawe mfano kwa wengine.

Awali, Mkurugenzi Mzawa wa Kampuni hiyo, Richard Sinamtwa, amesema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali licha ya kampuni hiyo kutoa ajira kwa zaidi ya vijana 10,000 ambao ni wakazi wa Manispaa ya Morogoro.

Amesema moja ya changamoto hizo ni kutishiwa kukamatwa na polisi bila sababu wawekezaji kutoka nje ya nchi kwa lengo la askari hao kutaka rushwa.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post