WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI NA KUJIEPUSHA NA RUSHWA


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Watumishi wa Umma kote nchini wametakiwa  kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma na kujiepusha na masuala ya rushwa na utovu wa nidhamu kazini. 


Rai hiyo imetolewa  Mei 14,2019  jijini Dodoma na Naibu katibu mkuu Utumishi, Bw.Francis Michael katika ufunguzi wa  mkutano Mkuu wa Mwaka wa Baraza la wafanyakazi wa ofisi ya Taifa ya Ukaguzi hesabu za Serikali C.A.G. 


Bw.Michael amesema kuna baadhi ya watumishi wa Umma wamekuwa wakikiuka maadili ya kazi na taaluma zao na kujikita wakiwa watovu wa nidhamu na kujikita kwenye masuala ambayo yako kinyume na utaratibu wa kazi hivyo ni vyema kwa kila mfanyakazi akazingatia maadili ya kazi zake. 


Hata hivyo,Bw.Francis ameipongeza ofisi ya ukaguzi wa hesabu za serikali ,C.A.G ikiongozwa na  kiongozi wake Mahiri Profesa Musa Assad kwa kuendelea kutoa ripoti  ya ukaguzi kwa wakati kila mwaka bila upendeleo wowote katika kusukuma gurudumu la Maendeleo kwa  kuelekea  Uchumi wa kati wa Tanzania ya  viwanda. 


Kuhusu changamoto zinazoikabili ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za serikali C.A.G hususan upungufu wa wafanyakazi Bw.Francis amesema ofisi yake ipo tayari kutatua tatizo hilo ambapo ameitaka ofisi ya C.A.G kufanya mchakato wa kuorodhesha idadi husika ya upungufu huo. 


Katibu wa TUGHE Taifa Heri Mkunda amezungumzia juu ya Ushirikishwaji wa wafanyakazi  katika bajeti ili kujenga dhana ya utawala bora . 


Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi ofisi ya Taifa ya ukaguzi C.A.G Prof.Musa Assad  amesema ofisi yake ina watumishi 957  huku kukiwa na upungufu wa watumishi zaidi ya hamsini  kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kustaafu,kufariki au kuhamishwa taasisi nyingine.

Kaulimbiu ya mkutano  mkuu wa mwaka wa Baraza la Wafanyakazi  ya ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ni Ukaguzi Shirikishi ,Uwazi na Uwajibikaji ni nguzo muhimu katika kufikia uchumi wa kati.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post