WALIMU WATAKIWA KUTODAI NYONGEZA YA MISHAHARA KAMA HAIJATOLEWA

Serikali imesema walimu hawapaswi kudai nyongeza ya mwaka ya mshahara kwa miaka ambayo nyongeza hiyo haikutolewa.


Hayo yamesemwa bungeni leo, Ijumaa Mei 10, na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Zainab Mussa Bakar (Chadema).

Katika swali lake Zainabu aliuliza; “Walimu nchini wameingia mkataba na mwajiri wao ambao pamoja na mambo mengine unaonyesha uwepo wa nyongeza ya mshahara kila ifikapo Julai, lakini tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani hawajapewa stahiki hizo, je ni lini walimu watalipwa malimbikizo hayo?”

Katika majibu yake, Waitara alisema Serikali imekuwa ikitekeleza miongozo mbalimbali kuhusu maslahi ya walimu zikiwamo nyongeza za mwaka za mishahara kulingana na utendaji wa mhusika na tathmini ya kila mwaka.

“Kwa mujibu wa kanuni E.9 (1) ya kanuni ya kudumu katika utumishi wa umma za mwaka 2009 toleo la tatu, nyongeza ya mwaka ya mshahara haipaswi kuombwa au kudaiwa na walimu, bali serikali ndiyo yenye uamuzi wa kutoa au kutotoa nyongeza hiyo kutokana na sera za kibajeti kwa mwaka husika." Amesema.


Amesema nyongeza hiyo haikutolewa kwa watumishi katika miaka 2003/2004 hadi 2016/17, lakini imetolewa kwa watumishi wote wakiwamo walimu mwaka wa fedha 2017/18.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post