SERIKALI YASEMA POLISI HAWATOWI FEDHA KUNUNUA CHAKULA CHA MAHABUSU


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamadi Masauni amesema  hakuna utaratibu wa askari polisi kutoa fedha zao mfukoni kwa ajili ya chakula cha mahabusu.

Kauli hiyo aliitoa jana bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Masasi, Rashid Chuachua (CCM).

Katika swali lake Mbunge huyo alitaka kujua serikali ni lini itarekebisha utaratibu uliopo ambapo askari wanalazimika kutoa pesa zao mfukoni ili kuwapa chakuka mahabusu.

Masauni alisema utaratibu uliopo  ni kwa serikali kupitia Jeshi la Polisi ina wajaibu wa kuwapatia chakula mahabusu waliopo  selo

“Ndugu wa Mahabusu pia wanaruhusiwa kupeleka chakula kwa mahabusu wao ambao wapo korokoroni,” alisema Masauni .

Alisema serikali inatambua uhaba wa vitendea kazi kwa Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja uchache wa  magari na nyumba za askari.

Alisema kwa sasa Wilaya ya Masasi ina nyumba za makazi ya askari zipatazo 15 ambazo zinaishi familia 30.

Alisema ni kweli askari wengine 154 bado wanaishi uraiani lakini hata hivyo serikali itaendelea kujenga nyumba za makazi ya askari kwa awamu kwa kadri ya upatikanaji wa fedha.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527