SERIKALI YAANZA KUSAMBAZA GESI ASILIA MTWARA, LINDI, PWANI NA DAR ES SALAAM


Serikali  imeanza kutekeleza mradi wa kusambaza gesi asilia katika miji ya Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es Salaam ikiwa ni nishati mbadala   kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu Mgalu aliyasema hayo  bungeni jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibiti, Ally Ungando (CCM).

Katika swali lake, Ungando  alihoji Serikali inamkakati gani wa kupeleka nishati mbadala katika Jimbo lake ikiwa ni pamoja ni aina  gani ya nishati itakayotumika badala ya kuni na mkaa.

Mbunge huyo alisema  wananchi wanaoishi katika Jimbo la Kibiti hutumia   kuni kwa matumizi ya nyumbani, shuleni, gerezani hivyo husababisha uharibifu mkubwa wa mazingira kwa kukata miti hovyo .

‘Je serikali inamkakati gani wa kupeleka nishati mbadala? Na je ni aina gani ya nishati itakayotumika badala ya kuni na mkaa?” aliuliza Ungando.

Akijibu, Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu, alisema  Mei 18 mwaka 2018 serikali kupitia Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) ilisaini mkataba wa kampuni ya Mihan Gas kwa ajili ya kusambaza vifaa vya kupikia mitungi ya gesi na majiko kwa watumishi wa umma na wananchi wengine   mpango  unaolenga kupunguza matumizi ya mkaa na kuni.

 Mgalu alisema   Sera ya Taifa ya Nishati ya Mwaka 2015 imetoa muongozo wa kuboresha maisha ya wananchi kwa matumizi bora ya nishati kupitia teknolojia ya kisasa badala ya kuni na mkaa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527