Picha : AGAPE YAKUTANA NA WATENDAJI WA SERIKALI KISHAPU KUJADILI SAUTI YA MWANAMKE NA MTOTO
Shirika lisilo la kiserikali AGAPE AIDS CONTROL PROGRAM Mkoani Shinyanga, limekutanisha watendaji wa Serikali kutoka halmashauri ya wilaya ya Kishapu pamoja na mkoa, kwa ajili ya kujadili namna ya kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.


Kikao hicho kimefanyika leo Mei 17,2019 katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya Liga Shinyanga Mjini, kwa kukutanisha Maofisa Maendeleo ya jamii wilaya ya Kishapu, watendaji wa Kata, maofisa ustawi wa jamii, mahakimu, wanasheria, dawati la Jinsia, pamoja na baadhi ya madiwani.

Akizungumza kwenye kikao hicho wakati akiwasilisha mradi wa Sauti ya Mwanamke na Watoto, Ofisa mradi kutoka Shirikala Agape Felex Ngaiza, amesema wamekutanisha watendaji hao wa serikali pamoja na baadhi ya madiwani kutoka kata tatu mahali ambapo mradi huo unatekelezwa, ili kuunganisha nguvu ya pamoja kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Amesema watendaji hao wa serikali ni wa muhimu sana katika kuendeleza mapambano ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, hali ambayo imewafanya kukaa nao kikao ili kuwaelezea namna mradi unavyofanya kazi pamoja na kutatua changamoto zake.

Amesema mradi huo utatekelezwa katika kata tatu za halmashauri ya wilaya ya Kishapu ambazo ni Itilima, Bunambiu na Kishapu, ambapo utatekelezwa kwa majaribio ndani ya miezi sita kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, na ukileta matokeo chanya utadumu ndani ya miaka mitano.

“Mradi huu wa Sauti ya Mwanamke na Mtoto ni wa miezi sita tu, ambao uzinduzi wake ulifanyika Aprili 9 mwaka huu, na umelenga kutokomeza masuala ya matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kwa kutolewa taarifa za matukio hayo na kuweza kuchukuliwa hatua za kisheria,”amesema Ngaiza.

“Matarajio ya mradi huu ni kuongeza uelewa wa kisheria kwa wanawake na watoto dhidi ya matukio ya kikatili ambayo hufanyiwa, utoaji wa taarifa nyingi za mtukio ya ukatili, pamoja na hatua za kisheria zipate kuchukuliwa dhidi ya watu ambao hufanya vitendo hivyo vya ukatili,”ameongeza.

Katika hatua nyingine Ngaiza ametaja changamoto ambazo wanakumbana nazo katika utekelezaji wa mradi huo, kuwa uongozi wa vijiji kukaa na kesi za matukio ya ukatili wa kinjsia kwa muda mrefu bila kuzipeleka kwenye mamlaka husika, na nyingine kuzifanyia suluhu bila ya kuwa na uwezo nazo, pamoja na ukosefu wa bajeti ya kuhudumia wahanga wanaofanyiwa ukatili.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa  Shirika la Agape, Amani Peter, amewataka watendaji hao wa serikali kuwa na ushirikiano mzuri na wananchi pale wanapopewa taarifa za matukio ya ukatili ,pamoja na kuwa wasiri ili kutoka haribu ushahidi dhidi ya kesi hizo, ambapo mara nyingi watuhumiwa wamekuwa wakikimbia kusiko julikana hasa wa matukio ya ubakaji na upigaji mimba wanafunzi pamoja na wananchi kuogopa kutengwa.

Nao baadhi ya washiriki wa kikao hicho walilipongeza Shirika hilo kwa kuwakutanisha pamoja, na kutoa maadhimio kuwa elimu iendelee kutolewa kwa wananchi juu ya kuachana na matukio hayo ya ukatili kwa wanawake na watoto hasa kwa kuendekeza tabia ya mfumo dume.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Kaimu mkurugenzi wa Shirika la Agape Peter Amani akielezea namna walivyoanzisha mradi huo wa Sauti ya Mwanamke na Mtoto, ambao umelenga kutokomeza masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilayani Kishapu katika Kata tatu za Bunambiu, Itilima na Kishapu. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Afisa mradi wa Sauti ya Mwanamke na Mtoto kutoka Shirika la Agape Felex Ngaiza, akielezea mradi namna utakavyokuwa unatekelezwa katika Kata hizo Tatu za Kishapu, ambapo utadumu kwa muda wa miezi sita.

Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Kishapu Joseph Swalala akichangia mada kwenye kikao hicho na kushauri jamii iendelee kupewa elimu juu ya kupinga matukio hayo ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Afisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo akichangia mada kwenye kikao hicho na kuomba pia kuwepo kwa usiri hasa kwa watu ambao wamekuwa wakitoa taarifa za matukio hayo ya ukatili, ili kulinda usalama wake pamoja na kutovuja kwa taarifa za mtuhumiwa kukata kukamatwa na matokeo yake wanakimbia.

Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Itilima wilayani Kishapu Athumani Kitundu, akichagia mada kwenye kikao hicho na kuomba pia jamii ipewe elimu ya kutosha kuachana na masuala ya mfumo dume, pamoja na kutoa ushahidi Mahakamani ili watuhumiwa wapate kuchukuliwa hatua za kisheria ili kukomesha matukio hayo ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Mtendaji wa Kata ya Kishapu Nunya Chege akichangia mada kwenye kikao hicho ameilalamikia Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ambayo imekuwa ikwazo kwao katika utendaji kazi wa kuzia matuki ya ukatili dhidi ya watoto hasa kwenye upewaji wa mimba na ndoa za utotoni kwa kushindwa kuwa tia hatiani watuhumiwa.

Askali kutoka dawati la jinsia Polisi wilaya ya Shinyanga Joseph Christopher naye akichangia mada kwenye kikao hicho na kuwataka wananchi wawe wanatoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi juu ya matukio ya ukatili ili yapate kushughulikiwa na kubainisha usiri kwa jeshi hilo hua upo pamoja na kuwahikishia usalama wao watoa taarifa wote.

AfisaMaendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Kishapu Neema Godwin Mwaifuge naye akichangia mada kwenye kikao hicho.

Kaimu Ofisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga Octavian Kiwone akiongoza majadiliano kwenye kikao hicho.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha Shirika la Agape cha kujadili namna ya kuunganisha nguvu ya pamoja na watendaji wa Serikali na baadhi ya madiwani juu ya kupambana na tatizo la kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilayani Kishapu katika Kata tatu za Bunambiu,Itilima na Kishapu.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha Shirika la Agape cha kujadili namna ya kuunganisha nguvu ya pamoja na watendaji wa serikali na baadhi ya madiwani juu ya kupambana na tatizo la kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilayani Kishapu katika Kata tatu za Bunambiu,Itilima na Kishapu.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha Shirika la Agape cha kujadili namna ya kuunganisha nguvu ya pamoja na watendaji wa Serikali na baadhi ya madiwani juu ya kupambana na tatizo la kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilayani Kishapu katika Kata tatu za Bunambiu,Itilima na Kishapu.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha Shirika la Agape cha kujadili namna ya kuunganisha nguvu ya pamoja na watendaji wa Serikali na baadhi ya madiwani juu ya kupambana na tatizo la kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilayani Kishapu katika kata tatu za Bunambiu,Itilima na Kishapu.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha Shirika la Agape cha kujadili namna ya kuunganisha nguvu ya pamoja na watendaji wa Serikali na baadhi ya madiwani juu ya kupambana na tatizo la kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilayani Kishapu katika Kata tatu za Bunambiu,Itilima na Kishapu.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha Shirika la Agape cha kujadili namna ya kuunganisha nguvu ya pamoja na watendaji wa Serikali na Baadhi ya Madiwani juu ya kupambana na tatizo la kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilayani Kishapu katika Kata tatu za Bunambiu,Itilima na Kishapu.

Picha zote na Marco Maduhu-Malunde 1 Blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post