RAIS APIGA MARUFUKU PICHA ZAKE KUWEKWA OFISINI..ADAI URAIS SIYO UMAARUFURais wa Ukraine, Volodymyr Oleksandrovych Zelensky.

Rais mpya wa Ukraine, Volodymyr Oleksandrovych Zelensky amepiga marufuku picha yake kuwekwa kwenye ofisi za umma kwa kile alichodai kuwa Urais sio umaarufu.

Rais Zelensky amesema kuwa badala ya kuwekwa picha zake ukutani, kila mmoja aweke picha za watoto wake ili awe anaitazama kila anapofanya maamuzi.

"Ni marufuku kuning'iniza picha zangu kwenye Ofisi zote za Umma, u-Rais si umaarufu ama kuwekwa ukutani, badala yake kila mmoja wenu aweke picha za watoto wake awe anazitazama kila anapofanya maamuzi ya nchi hii", amesema Zelensky, Rais mpya wa Ukraine.

Volodymyr Oleksandrovych Zelensky, Rais mpya wa Ukraine alishinda katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika April 21. Kabla ya kuamua kugombea urais, Zelensky alikuwa msanii maarufu wa vichekesho nchini humo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post