Picha : DC MBONEKO AMWAGA VIFAA VYA SHULE KWA WATOTO WENYE UALBINO BUHANGIJA, AWASIHI WASOME KWA BIDII

Na Marco Maduhu - Malunde1 blog Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, ametoa msaada wa vifaa vya shule kwenye kituo cha kulea watoto wenye ulemavu ualbino Buhangija Jumuishi kilichopo manispaa ya Shinyanga, kwa ajili ya kuwapatia hamasa ya kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao.

Mboneko ametoa msaada huo leo Mei 25, 2019 akiongozana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, pamoja na Ofisa Maendeleo ya Jamii manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone, kwa kutoa msaada huo wa vifaa vya shule kwa watoto hao.
Amesema msaada wa vifaa hivyo vya shule ameshirikiana na marafiki zake wa Kikundi cha Digital Women cha Jijini Dar es salaam, ambapo wameguswa na watoto hao wenye ualbino, na kuamua kuwasaidia vifaa hivyo,ili kutoa hamasa kwao ya kusoma kwa bidii.
“Vifaa hivi vya Shule nimeshirikiana na marafiki zangu wa kikundi cha Digital Women cha jijini Dar es salaam, ambapo wameguswa  na ninyi na kuamua kuwasaidia ili msome kwa bidii na kutimiza ndoto zenu,”alisema Mboneko.
“Vifaa vya shule ambavyo nitawapatia ni madaftari, Counter Book, kalamu za penseli na wino, vifutio, vichongeo, rula, soksi, nguo za ndani kwa watoto wa kike na wa kiume, pamoja na zawadi zingine kama pipi na biskuti,” aliongeza.
Pia aliwapongeza walezi wa kituo hicho kwa kwahudumia watoto hao vizuri  na kuwalea kama watoto wao, huku akiwataka waendelea kuboresha hali ya usafi  kituoni hapo ili kuwaepusha na magonjwa ya mlipuko.
Naye mkuu wa kituo cha Polisi Shinyanga Mjini (OCS) Grace Salia, aliwahakikisha ulinzi na usalama watoto hao kwenye kituo hicho, ambapo siku zote wamekuwa wakilindwa na askari.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Buhangija Seleman Kipanya ambaye ndiye mlezi mkuu wa kituo hicho, akizungumza kwa niaba ya watoto hao alimpongeza mkuu huyo wa wilaya kwa kutoa vifaa hivyo vya shule pamoja na marafiki zake, ambavyo vitawasaidia katika masomo yao.
Alitaja jumla ya watoto ambao wanalelewa kwenye kituo hicho kuwa wapo 230, wasiosikia 74,Wasioona 36, pamoja na wenye ualbino 140 ambao ndiyo wengi zaidi, na kutoa wito kwa wadau wengine kuendelea kujitokeza ili kuwatatulia baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwataka watoto wenye ualbino wanaolelewa kwenye kituo cha Buhanghija Jumuishi Shinyanga Mjini wasome kwa bidii ili kutimiza Ndoto zao. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Askari Alphonce Bandya (ASP) kwa niaba ya Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga (RPC) Richard Abwao, akiwasisitiza watoto hao kupenda sana elimu ambayo ndiyo itakuwa mkombozi wa maisha yao.
Mkuu wa kituo cha Polisi Shinyanga Mjini (OCS) Grace Salia, akiwahakikisha ulinzi na usalama watoto hao wenye ualbino.
Watoto wenye Ualbino wakisikiliza nasaha za viongozi juu ya kusoma kwa bidiii.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akigawa vifaa vya shule kwa watoto wenye ualbino.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule kwa watoto wenye Ualbino.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule kwa watoto wenye Ualbino.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule kwa watoto wenye Ualbino.
Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akigawa vifaa vya Shule kwa watoto wenye Ualbino.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akigawa vifaa vya shule kwa watoto wenye Ualbino.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule kwa watoto wenye Ualbino.
Zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule kwa watoto  likiendelea.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule kwa watoto wenye Ualbino.
Zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule likiendelea kwa watoto hao wenye Ualbino.
Zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule likiendelea kwa watoto hao wenye Ualbino.
Zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule likiendelea kwa watoto hao wenye Ualbino.
Zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule likiendelea kwa watoto hao wenye Ualbino.
Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akigawa vifaa vya Shule kwa watoto wenye Ualbino.
Watoto wenye Ualbino wakiangalia Madaftari waliyopewa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko .
Watoto wenye Ualbino wakiangalia Rula ambazo wamepewa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Watoto wenye Ualbino wakionyesha vifaa vya Shule ambavyo wamepewa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Watoto wenye Ualbino wakionyesha Soksi kwa ajili ya kuvalia kwenye viatu vya shuleni.
Watoto wenye Ualbino ambao wapo darasa la Saba wakiangalia Counter Book walizopewa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akifungua boksi la biskuti kwa ajili ya kuzigawa kwa watoto wenye Ualbino.
Zoezi la ugawaji Piki na Biskuti likiendelea.
 Muonekano wa vifaa vya shule.
 Awali watoto wenye Ualbino wakimkaribisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wakati akiwasili kwenye kituo chao kwa ajili ya kuwapatia vifaa vya shule.
 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwaaga watoto hao wenye Ualbino mara baada ya kumaliza kutoa zawadi ya vifaa vya Shule na kuahidi Serikali itaendelea kuwa nao pamoja katika kuwatatulia changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili.
 Mwalimu mkuu wa Shule ya Buhanghija Selemani Kipanya ambaye pia ndiye mlezi mkuu wa watoto hao wenye Ualbino akishukuru kwa msaada huo wa vifaa vya shule ambavyo vitawasaidia watoto hao katika masomo yao.
 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, mkono wa kushoto akiwa na Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone wakikagua mahali ambapo wanalala watoto hao wenye Ualbino na kukuta hali ya usafi inaridhisha.
 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko katikati akiwa na Mkuu wa kito cha Polisi Shinyanga Grace Salia mkono wa kulia, huku mkono wa kushoto ni Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone, wakipiga picha ya pamoja na watoto wenye Ualbino.

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post