Picha : STEPHEN MASELE ARUDI TANZANIA BAADA YA MKUTANO WA BUNGE LA AFRIKA (PAP) KUFUNGWA


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mhe. Stephen Masele ambaye ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini amerudi nchini Tanzania baada ya Mkutano wa Bunge la Afrika uliokuwa unaendelea jijini Johannesburg,Afrika Kusini tangu Mei 6,2019, kufungwa leo Ijumaa Mei 17,2019.

Mhe. Masele ambaye ni Mkuu wa Utawala PAP alikuwa anahudhuria mkutano wa bunge la Afrika na baada ya kukamilisha majukumu yaliyompeleka sasa amerejea nyumbani Tanzania huku wabunge wengine waliokuwa wakishiriki mkutano nao wakirudi katika nchi zao.

Soma pia : Picha : MKUTANO WA PILI WA BUNGE LA AFRIKA (PAP) WAFUNGWA
Walinzi wakiwa wamebeba mizigo ya Mhe. Stephen Masele tayari kuelekea uwanja wa ndege.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mhe. Stephen  Masele akiondoka katika Hotel ya Gallagher hoteli iliyopo jijini Johannesburg,Afrika Kusini baada ya mkutano wa Bunge la Afrika kufungwa leo Mei 17,2019.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mhe. Stephen Masele.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527