MAREKANI YATUMA MFUMO WA KUKINGA MAKOMBORA NA MELI YA KIJESHI MASHARIKI YA KATI HUKU WASIWASI KATI YAKE NA IRAN UKIENDELEA


Marekani inatuma mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora na meli ya kivita katika eneo la mashariki kutokana na hali ya waiswasi iliopo katiya taifa hilo na Iran.

Meli hiyo ya kivita ya USS Arlington, inayosafirisha magari na ndege , itajiunga na kundi la kijeshi la USS Abraham Lincoln katika ghuba , maafisa wanasema.

Makombora ya US B-52 bombers pia yamewasili katika kambi moja nchini Qatar , idara hiyo imesema.

Imesema kuwa hatua hiyo inafuatia vitisho vya operesheni za vikosi vya kijeshi vya Marekani katika eneo hilo.

Marekani imetoa habari chache kuhusu uwezo wa tishio hilo , ambao Iran umepinga kama ujinga, ikitaja hatua hiyo ya Marekani kama vita vya kiakili vyenye lengo la kuitishia nchi hiyo.

Wakati huohuo chombo cha habari cha Isna News Agency kilimnukuu kiongozi mmoja mkuu wa dini , Yousef Tabatabai-Nejad akisema kuwa ''msafara huo wa Marekani unaweza kuharibiwa na kombora moja pekee''.

Siku ya Ijumaa idara ya Pentagon ilisema kuwa Marekani haitaki vita na Iran lakini Washington iko tayari kulinda vikosi vya Marekani na mali yake katika eneo hilo.

''Idara ya ulinzi inaendelea kufuatilia kwa karibu vitendo vya utawala wa Iran'', ilisema katika taarifa.

Iliongezea kuwa mfumo huo wa makombora ambao unaweza kutungua makombora ya masafa marefu na yale ya chini chini na ndege za kijeshi pia utapelekwa katika eneo hilo iwapo kuna uwezekano wa shambulio lolote.

Maafisa wameambia vyombo vya habari vya nchini Marekani kwamba meli hiyo ya USS Arlington ilitarajiwa kuwasili katika eneo hilo lakini imepelekwa katika eneo hilo mapema ili kutoa uwezo wa amri zitakazotolewa na udhibiti.

Siku ya Jumapili , mshauri wa maswala ya usalama nchini ,Marekani John Bolton amesema kuwa kupelekwa kwa vifaa hivyo vya kijeshi kutatoa ujumbe wa wazi kwa utawala wa Iran kwamba shambulio lolote dhidi ya mali ya Marekani katika eneo hilo litajibiwa na uwezo mkubwa wa kijeshi.

Meli hiyo ya USS Abraham Lincoln ilipita kupitia rasi ya Suez siku ya Alhamisi , kulingana na idara ya ulinzi nchini Marekani


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post