MAKONDA ATOA SADAKA ZAIDI YA MISIKITI 1,000


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Mhe. Paul Makonda leo amewakabidhi shehena ya viungo vya kutengeneza futari kwa maimamu, mashehe na viongozi wa Dini ya Kislamu kutoka Misikiti zaidi ya 1,000 kama sehemu ya sadaka na shukrani ya Amani na Utulivu ndani ya mkoa huo.


Miongoni mwa vitu alivyokabidhi RC Makonda ni Mchele, Sukari, Unga, Maharage, Mafuta na vitu mbalimbali kwaajili ya kuwawezesha viongozi hao kufurahia futari majumbani mwao.

RC Makonda amewashukuru viongozi wa dini kwa kuwa wasimamizi wazuri wa Amani na mshikamano ndani ya mkoa huo jambo linalofanya mkoa huo kuendelea kuwa kisima cha Amani.

Hata hivyo RC Makonda amewaeleza Viongozi wa Dini kuwa namna bora ya kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli na kumuombea ni kuhakikisha waumini wao wanajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili wachague viongozi wa serikali za mitaa wanaochukia Rushwa.

Aidha RC Makonda amemshukuru Balozi wa Falme za Kiarabu kwa kumkabidhi misaada hiyo huku akiwasihi waislamu kutumia mfungo huu Kuliombea taifa na viongozi pamoja na kuwahimiza wazazi kuwalea watoto katika malezi bora.

Kwa upande wake Balozi mdogo wa Falme za Kiarabu amesema wameamua kumuunga mkono RC Makonda kwakuwa wanamuamini akipokea kitu kinawafikia walengwa na amekuwa mtu wa kuwasaidia watu wasiojiweza bila kujali dini wala kabila.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post