Picha : RAIS MAGUFULI ATUA AFRIKA KUSINI KUHUDHURIA SHEREHE YA UAPISHO WA RAIS MTEULE CYRIL RAMAPHOSA


Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa OR Tambo Nchini Afrika Kusini kwaajili ya kuhudhuria Sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa nchi hiyo Mhe.Cyril Ramaphosa ambaye anatarajiwa kuapishwa Mei 25,2019. Picha na Ikulu




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya kuingia kwenye ndege ya Shirika la ndege la Tanzania (Air Tanzania) walipokuwa wakielekea Nchini Afrika Kusini kwaajili ya Sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa nchi hiyo Mhe.Cyril Ramaphosa ambaye anatarajiwa kuapishwa Mei 25,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa kwenye ndege ya Shirika la ndege la Tanzania (Air Tanzania) wakielekea Nchini Afrika Kusini kwaajili ya Sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa nchi hiyo Mhe.Cyril Ramaphosa ambaye anatarajiwa kuapishwa Mei 25,2019.

Picha na Ikulu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527