MBUNGE WA ESWATINI AKANUSHA TAARIFA ZA MFALME MSWATI KUAGIZA WANAUME KUOA WANAWAKE WAWILI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, May 15, 2019

MBUNGE WA ESWATINI AKANUSHA TAARIFA ZA MFALME MSWATI KUAGIZA WANAUME KUOA WANAWAKE WAWILI

  Malunde       Wednesday, May 15, 2019
Mbunge wa Bunge la Afrika kutoka Eswatini Mhe. Mike Temple akizungumza katika Mkutano wa Bunge la Afrika unaoendelea Jijini Johannesburg,Afrika Kusini leo - Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
 ****
Serikali ya nchi ya Eswatini imekanusha taarifa zinazoenea kwa kasi mtandaoni kuwa Mfalme Mswati III ametoa agizo la wanaume nchini humo kuanzia Mwezi Juni 2019 kuoa wanawake wawili au zaidi la sivyo unatupwa jela. 

Akizungumza leo asubuhi Jumatano Mei 15,2019 katika Bunge la Afrika linaloendelea jijini Johannesburg,nchini Afrika Kusini,Mbunge wa Eswatini, Mhe. Michael Temple amesema ni vyema taarifa hizo zikapuuzwa kwani zina lengo la kumchafua Mfalme Mswati III. 

“Mhe.Rais wa Bunge la Afrika,kabla ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Bunge la Afrika ya mwaka 2018 na bajeti iliyopendekezwa ya Bunge la Afrika kwa mwaka 2020,naomba kuweka sawa jambo moja ambalo linasambaa sana mtandaoni kuwa Mfalme wetu ametangaza kuwa wanaume waoe wanawake wawili au zaidi”,ameeleza Mhe. Temple ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Usimamizi wa Mambo ya Fedha Bunge la Afrika. 

“Kwa niaba ya Mfalme wetu,naomba kuliambia bunge hili kuwa,Mfalme wetu siyo dikteta na haongozi kwa matamko,na hakuna sheria ya kumlazimisha mtu kuoa..hivyo hajasema na wala hategemei kusema hicho kinachoenezwa, huu ni uongo mtupu unaolenga kumchafua Mfalme wetu”,amesema Mhe. Temple. 

“Tuondoe huu upepo unaoenea na kuchafua nchi na Mfalme wetu,mimi mwenyewe hapa nina mke mmoja tu,na hakuna sheria inayomlazimu mtu kuoa, kuoa ni maamuzi ya mtu binafsi kuchagua kuoa au la”,ameongeza Mhe. Temple.

Na Kadama Malunde – Malunde1 blog 

Mbunge wa Bunge la Afrika kutoka Eswatini Mhe. Mike Temple akizungumza katika Mkutano wa Bunge la Afrika unaoendelea Jijini Johannesburg,Afrika Kusini leo - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Wabunge wakiwa ukumbini .Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post