KOREA KASKAZINI YARUSHA KOMBORA HUKU MJUMBE WA MAREKANI AKIWASILI KOREA KUSINI


Korea Kusini imesema jirani yake Korea Kaskazini imerusha kombora lingine leo ikiwa ni mara ya pili wiki hii. 


Kombora hilo limerushwa ikiwa ni masaa machache kabla baada ya kuwasili mjini Seoul, Mjumbe Maalum wa Marekani kwa Korea Kaskazini, Stephen Biegun, kwa mazungumzo na maafisa wa Korea Kusini kuijadili Korea Kaskazini na mpango wake wa makombora na silaha za nyuklia. 

Jumamosi iliyopita, Korea Kaskazini pia ilifanya zoezi la kijeshi na kurusha makombora kadhaa, mojawapo likiaminiwa kuwa ni la masafa mafupi. 

Ni ziara ya kwanza ya Biegun mjini Seoul, tangu mkutano wa kilele wa Hanoi kati ya Marekani na Korea Kaskazini kumalizika bila ya mafanikio. 

Katika mkutano huo, Kim Jong-un alisema atasitisha mpango wake wa nyuklia pale Marekani itakapoiondolea nchi yake vikwazo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527