KONDOO WAANDIKISHWA SHULE ILI KUJAZA NAFASI YA WANAFUNZI DARASANI

Mkulima mmoja nchini Ufaransa amewaandikisha shule kondoo wake 15 ili kuongeza namba ya wanafunzi baada ya mamlaka za kijiji kimoja kutangaza kutaka kusitisha masomo.

Shule ya Jules Ferry iliyopo kwenye kijiji cha CrĂȘts-en-Belledonne, kwenye safu za milima ya Alps karibu na jiji la Grenoble, kimekuwa kikikumbwa na tatizo la kushuka kwa namba ya wanafunzi wanaoandikishwa kwa masomo.

Hali hiyo inatishia kufungwa kwa shule hiyo.

Lakini kama hatua ya kupinga kufungwa kwa shule, mfugaji na mkulima Michel Girerd ameamua kuwaandikisha baadhi ya kondoo wake kama wanafunzi.

Baadhi ya kwanafunzi hao ambao ni kondoo wanafamika kwa majina kama Baa-bete, Dolly na Shaun.
Bw Girerd alienda shuleni hapo akiwa na kondoo 50 kuhudhuria sherehe maalumu iliyohudhuriwa na watu 200 wakiwemo wanafunzi, walimu na maafisaa wengine.

Meya wa eneo hilo, Jean-Louis Maret alikabidhiwa vyeti vya kuzaliwa vya 'wanafunzi' hao wapya. Pia akaonesha kukerwa kwake na suala la kutishia kufunga shule hiyo kutokana na uhaba wa wanafunzi.

"Sasa hakutakuwa na tishio la kufungwa kwa kitu chochote," moja ya wazazi Gaelle Laval amesema, na kuongeza kuwa mfumo wa elimu "hauangalii hoja zilizopo katika eneo hilo, na badala yake unaangalia idadi (ya wanafunzi) tu."

Wanafunzi waliohudhuria sherehe hiyo walibeba mabango yalikuwa na ujumbe kuwa: "Sisi siyo kondoo".

Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post