RIDHIWANI KIKWETE ATOA MISAADA KATA YA UBENA ZOMOZI - CHALINZE


Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh.Ridhiwani Kikwete akimkabidhi msaada wa Baiskeli ya Miguu mitatu (Wheel Chair),Mkazi wa Zomozi-Ubena Mzee Cosmas Alphonce Chongwe ambaye ni mlemavu wa miguu,leo baada ya Mbunge huyo kumaliza kikao chake alichofanya pamoja na Wajumbe wa Mkutano mkuu wa CCM wa Kata ya Ubena-Zomozi,Chalinze.

Mh.Ridhiwani amekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya saruji 20 kwa ajili ya uanzishwaji ujenzi wa shule ya Msingi katika kitongoji cha Choza,Matofali Elfu tatu,fimbo nne maalum kwa ajili ya walemavu wa macho,Kadi 23 za Afya kwa ajili ya matibabu ya wazee, vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi Milioni tano.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh.Ridhiwani Kikwete akimuelekeza Mkazi wa Zomozi-Ubena Mzee Cosmas Alphonce Chongwe ,ambaye ni mlemavau wa Miguu namna ya kutumia Baiskeli ya Miguu mitatu (Wheel Chair),aliyomkabidhi kama msaada.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh.Ridhiwani Kikwete akimkabidhi fimbo maalum kwa ajili ya walemavu wa macho,Josephat Mgonge,ambaye ni mlemavu wa macho.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh.Ridhiwani Kikwete akikabidhi mfuko wa saruji kwa uongozi wa chama cha CCM,ambapo Mh.Mbunge msaada wa mifuko ya saruji 20 na matofali 3,000 kwa ajili ya uanzishwaji ujenzi wa shule ya msingi katika kitongoji cha Choza.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh.Ridhiwani Kikwete akikabidhi kadi ya matibabu maalum kwa Wazee,Mzee Ally Gola,ambapo kadi 25 zilitolewa kwa Wazee.
Mmoja wa Wazee akimshukuru Mbunge Ridhiwani Kikwete kwa kuwapatia msaada wa kadi za matibabu,kulia ni Diwani wa Kata ya Ubena-Zomozi,Nicholaus Muyuwa akishuhudia.

Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze 
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ametoa msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya saruji 20 na matofali 3,000 kwa ajili ya uanzishwaji ujenzi wa shule ya msingi katika kitongoji cha Choza.

Aidha amemkabidhi msaada wa baiskeli ya miguu mitatu (wheel Chair),mkazi wa Zomozi-Ubena mzee Cosmas Alphonce Chongwe ambae ni mlemavu wa miguu.

Katika hatua nyingine ,Ridhiwani alitoa fimbo nne maalum kwa ajili ya walemavu wa macho,kadi 23 za afya kwa ajili ya matibabu ya wazee, vyote vikiwa na thamani zaidi ya sh.milioni tano.

Mbunge huyo alitoa misaada hiyo baada ya kumaliza kikao chake alichofanya pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Ubena-Zomozi.

Ridhiwani alieleza, msaada huo alioutoa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Ilani ya uchaguzi na maombi mbalimbali ya wananchi katika kata hiyo. 

Pamoja na hayo, alikutana na wanachama mbalimbali wa vikundi vya maendeleo katika kata hiyo, ambapo aliwahimiza kuendelea kujiunga vikundi ili kuweza kupata mikopo kirahisi na kuwezeshwa kuliko kuwa mmoja mmoja. 

Hakusita kusema, ataendelea kusaidia makundi maalum na kusimamia kero zinazowakabili wananchi wa jimbo la Chalinze.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post