BASI LA NEW FORCE LAGONGANA NA LORI NA KUUA,KUJERUHI


Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 15 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la New Force lililogongana na lori kati ya eneo la Mafinga na Nyololo mkoani Iringa leo Jumapili Mei 19, 2019.

 Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamhuri William amesema ajali hiyo imetokea kwenye misitu ya Sao Hill, na dereva wa lori amefariki dunia papo hapo.

Ajali hiyo imehusisha basi la New Force lililokuwa likitoka jijini Dar es Salaam kwenda jijini Mbeya na liligongana na lori hilo lililokuwa limeingia ghafla barabarani likitokea kwenye barabara ya mchepuko.

“Bado tunaendelea kuchambua idadi ya majeruhi lakini hadi sasa aliyefariki dunia katika ajali hiyo ni mtu mmoja ambaye ni dereva wa lori lililohusika kwenye ajali hiyo, idadi ya majeruhi hadi sasa ni 15,” amesema mkuu huyo wa wilaya.

Amesema baadhi ya majeruhi wamepelekwa hospitali ya Mafinga kwa matibabu kutokana na majeraha waliyopata kwenye ajali hiyo.

ANGALIA <<VIDEO>> HAPA
CHANZO - MWANANCHI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527