KAMPUNI YA INFINIX NA TIGO YALETA MAPINDUZI YA SELFIE KUPITIA INFINIX S4 YENYE 32MPKampuni ya simu ya Infinix inayozalisha simu zenye teknolojia ya hali ya juu, imezindua simu mpya aina ya Infinix S4 yenye megapixel 32 AI selfie kwajili ya kuwawezesha watanzania kufikia ndoto zao kupitia matumizi ya teknolojia. Na kwa ushirikiano wa TIGO na Infinix, Infinix S4 itapatikana katika maduka ya Infinix na TIGO ikiwa na ofa ya bundle la miezi sita.   


Infinix na Tigo zimeungana katika uzinduzi wa Infinix S4 kuhakikisha wateja na Watanzania kwa ujumla wanaingia katika mapinduzi ya simu zenye selfie bora, ambayo sio tu itainua ujuzi na maarifa ya selfie lakini pia itasaidia kuwasogeza katika ulimwengu wa kidigitali. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi Mkurugezi mtendaji wa kampuni ya simu ya Infinix Bwana. Hauson Tu,alisema kwamba, “Uwezeshaji kupitia teknolojia ya simu unategemeana na uhakika wa sifa ya simu kama vile kamera ya nyuma, mwonekano mzuri wa screen ya simu, uwezo wa betri na kasi ya simu yenyewe. Kwa kulizingatia hilo Infinix S4 imeundwa ikiwa na kamera tatu za nyuma 13MP+8MP+2MP with a 6.2’ waterdrop display screen kwaajili ya picha bora. Kamera hizi tatu zenye kufanya kazi tatu tofauti ikiwemo kuhakikisha picha inaonekana kwa kina zaidi, hata kwa umbali wa 120ยบ”. 

Bwana Tu, “alisisitiza kuhusu umuhimu wa Betri yenye nguvu inayodumu na chaji zaidi akisema, “Infinix haijawahi kuwaangusha wateja wake katika suala la betri. S4 ina Smart power management system kwaajili ya kuzuia matumizi ya chaji kwa application ambazo hazitumiki kwa muda huo na betri hutumika pale tu ambapo application hiyo itakuwa katika matumizi”. 

Na kwa upande wake afisa mahusiano wa kampuni ya Tigo Bwana Tarik Boudiaf alisema “Kasi ya mtandao ni muhimu sana katika kumwezesha Mtanzania, ikiwa ni lengo mojawapo kwa kampuni ya Tigo kuhakikisha wateja na Watanzania kwa ujumla wanahamia katika ulimwengu wa kidigitali kama kampuni tumetoa ofa ya bundle la internet la muda wa miezi sita”. 

Kampuni ya simu ya Infinix imekuwa ikiwalenga zaidi vijana na watu wenye ushawishi katika maendeleo ya teknolojia, hii imepelekea uzinduzi wa Infinix S4 kuhudhuriwa na wasanii maaruufu kama Lulu Diva, Mimi Mars, Bi Dozen pamoja na vyombo vya habari maarufu. Infinix S4 kwa sasa inapatikana katika maduka yote ya Infinix na TIGO Nchini kote.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post