BABU WA MIAKA 65 ACHAPWA VIBOKO NZEGA ,ASUKUMWA JELA MAISHA


Na Lucas Raphael, Tabora 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Nzega mkoni Tabora imemhukumu kifungo cha maisha jela na kumchapa viboko sita mkazi wa mtaa wa National Hausing, Juliasi Katambi (65) baada ya kumnajisi mtoto mwenye umri wa miaka sita mwanafunzi wa Shule ya Msingi Nyasa Mbili iliyopo Nzega Mjini.

Akitoa hukumu hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nzega, Gradness Badha alisema kuwa kutokana na ushahidi usioacha shaka, mahakama hiyo imeridhia kumpa adhabu hiyo Katambi ili kutumikia kifungo hicho baada ya mashahidi watano kutoa ushahidi juu ya tukio hilo la ubakaji.

Hakimu huyo alisema kuwa kutokana na kitendo hicho cha kinyama, mahakama hiyo imetoa hukumu iyo ili iwe fundisho kwake na kwajamii hasa kwa watu wenye kuendekeza vitendo hivyo vya ukatili kwa watoto wa kike na wanawake.

Awali, Wakili wa Serikali Piter Utafu aliieleza makahama hiyo kwamba mnamo Aprili 22, mwaka 2018 majira ya jioni katika maeneo ya Shule ya Msingi Nyasa Mbili iliyopo Nzega Mjini, mwanafunzi huyo alibakwa kwa nguvu na Katambi mwenye umri wa miaka 65 na kumsababishia maumivu makali katika mwili wake.

Wakili huyo alisema kutokana na kitendo hicho na upelelezi kukamilika na mashahidi watano kutoa ushahidi wa kuridhidha mahakamani hapo ni vema mahakama ikatoa adhabu kali kwa Katambi ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye nia na tabia kama hizo.

Mahakama ilitoa nafasi ya utetezi kwa mshitakiwa huyo baada ya kupatikana na hatia ambapo aliomba kupunguziwa adhabu kwa vile ni mara yake ya kwanza kutenda kosa kama hilo na vile vile ana umri mkubwa.

Hata hivyo, Mahakama ya Wilaya ya Nzega haikuridhika na utetezi huo na kumhukumu kutumikia kifungo cha maisha jela na kuchapwa viboko sita.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post