HAKIMU WA MAHAKAMA WILAYA NA MAWAKILI WA SERIKALI KIZIMBANI ARUSHA

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Hakimu wa mahakama ya wilaya mkoani Arusha Benard Nganga,na wenzake wanne wakiwemo mawakili wa serikali wamepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka kumi na moja yakiwemo ya uhujumu wa uchumi na utakatishaji wa fedha.


Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu mfawidhi Niku Mwakatobe wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha Mwendesha mashtaka wa serikali Javelin Rugailuza amewataja washtakiwa wengine ni Maneno Mbunda wakili wa shirika la hifadhi za Taifa (Tanapa),Fortunatus Mhalila na Tumaini Mdee wote ni mawakili wa serikali na mfanyabiashara Nelson Kangero.

Mwendesha mashtaka huyo ameeleza kuwa kati ya tarehe 1 mwezi wa sita mwaka 2018 katika maeneo tofauti jijini Arusha na mkoani Arusha washtakiwa kwa pamoja walitenda makosa mbali mbali ya uhujumu wa uchumi na kujipatia rushwa na uundwaji wa genge la mtandao wa uhalifu.

Makosa mengine wanayokabiliana nayo ni pamoja na kutoa na kupokea rushwa ya million 31.5 kwa lengo la kushawishi wa kuwezesha kuwachiwa huru kwa mhalifu na ,kuhuaribu ushahidi, na kuchoma jalada la kesi,pamoja na kuwasilisha nyaraka za uongo.

Baada ya mwendesha mashtaka huyo kuwasomea mashataka hayo hawakutakiwa kujibu chochote kwani mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo hivyo kuahirishwa hadi tarehe 20 mwezi huu.

Wakati huo huo Mshatakiwa Nelson Kangero alisomewa shatka mmoja la kukutwa na meno 15 ya Tembo ambayo ni nyara za serikali zenye thamani ya million 100.8 kinyume cha sheria.

Akisoma shtaka hilo mbele ya hakimu mfawidhi Mwakatobe Mwendesha mashtaka wa serikali Javelin Rugailuza alisema kuwa mnamo disemba 15 mwaka 2017 katika eneo la kichwa cha nyumbu Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro mtuhumiwa alikutwa na Meno ya tembo yenye thamani ya dola za Kimarekani 15000 mali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo hivyo kupelekwa rumande hadi mei 20 mwaka huu kesi itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Makosa ya jinai wa Jeshi la Polisi (DCI)Robert Boaz amesema kuwa hali ya uhalifu nchini imepungua kwa asilimia 3.4 ukilinganisha na makosa kama hayo mwaka jana ambayo yalikuwa 14,866 na robo mwaka huu ni 14,355.

Akizungumzia makosa makubwa yakiwemo ya Unyang’anyi wa kutumia silaha na Ujangili Boaz alisema yamepungua kwa asilimia 4.7 ambapo mwaka jana yalikuwa 6897 na mwaka huu ni makosa 6573,hatua hiyo imetokana na Jeshi hilo kuunda timu ya kufuatilia uhalifu na kufanikisha mbaroni wa husika na vifaa vyao vya kazi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527