Picha : AGAPE YAKUTANA NA VIONGOZI WA JAMII USANDA KUWAPA NONDO ZA KUENDELEZA VITA DHIDI YA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI

Shirika lisilo la kiserikali la mkoani Shinyanga AGAPE ACP, limeendesha kikao kwa viongozi wa jamii 30 wakiwemo wenyeviti wa vitongoji 30,viongozi wa kidini na kimila, wazee maarufu na waelimishaji rika kwenye  kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuendeleza mapambano ukatili dhidi ya wanawake na watoto.Kikao hicho kimefanyika leo Mei 22, 2019 katika shule ya msingi Singita kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ambapo mgeni rasmi alikuwa Afisa mtendaji wa kata hiyo Emmanuel Maduhu, ambapo amewataka viongozi hao kuwa mstari wa mbele kupambana na matukio ya ukatili ndani ya jamii, ikiwamo kutokomeza mimba
na ndoa za utotoni.

Akizungumza kwenye kikao hicho Mratibu wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape mkoani Shinyanga Lucy Maganga, amesema mradi huo unaelekea ukingoni ambapo ulianza (2017) na kutarajiwa kuisha Julai 2019, ambapo walianza kwa kuwajengea uwezo viongozi hao namna ya kuendelea kupambana kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Amesema wameamua kuendesha kikao hicho kwa viongozi hao ambao ndiyo wapo karibu na wananchi zaidi muda wote, kwa kuwapatia elimu namna ya kutokomeza matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto, licha ya mradi wao huo kukoma ambapo elimu itakuwa ikizidi kutolewa ndani ya jamii na hatimaye kuishi salama.

“Mradi wetu huu umekaribia kuisha kutekelezwa katika kata hii ya Usanda,ambao ulikuwa wa miaka miwili na utakoma Julai 2019, hivyo kutokana na mafanikio yaliyopatikana ikiwemo kupunguza matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto zikiwamo mimba na ndoa za utotoni, tukaona pia tuwajengee uwezo viongozi hawa ambao wataendeleza gurudumu la kutokomeza kabisa matukio haya,”amesema Maganga.

“Kikao chetu hiki cha leo kimeshirikisha wenyeviti wa vitongoji 30 wa kata ya Usanda, waelimishaji rika, wazee maarufu, wazee wa kimila, ambapo wamepewa elimu namna
ya kupambana kutokomeza matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto zikiwamo mimba na ndoa za utotoni ili kuendeleza kupinga ukatili ndani ya jamii,” ameongeza.

Naye mgeni rasmi mtendaji huyo wa kata ya Usanda Emmanuel Maduhu, amewataka wenyeviti wa
vitongoji kwenye kata hiyo elimu ambayo wamepewa wakaitumie vizuri katika kutokomeza matukio hayo ya ukatili kwa wanawake na watoto, na kuzuia ndoa za utotoni kwa kufanya uchunguzi kama binti anayeolewa si chini ya umri
wa miaka 18.

Amesema wenyeviti wa vitongoji ndiyo wanaishi karibu zaidi na wananchi na wanawafahamu kila mmoja na kaya yake, hivyo wanamchango mkubwa katika kupunguza ama kumaliza kabisa matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto likiwamo na suala la mimba na ndoa za utotoni, kwa kusimamia hata sheria za kimila kwa kuwatenga wale ambao
bado wanaendekeza vitendo hivyo.

Kwa upande wake Ofisa elimu wa kata ya Usanda Sospeter Kasonta, amelipongeza Shirika hilo la Agape ambalo limekuwa na mchango mkubwa katika sekta ya elimu na afya, kwa kuibadilisha jamii kupenda kusomesha watoto wao pamoja na wanafunzi wenyewe kujitambua, ambapo ufaulu wa wanafunzi umeongezeka hasa wa kike tofauti na
kipindi cha nyuma.

Nao baadhi ya washiriki wa kikao hicho akiwemo Daudi Shija kutoka kitongoji cha Uswahilini  amesema mafunzo hayo watayatumia vizuri na kuleta matokeo chanya ndani ya jamii, ili kupunguza matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Mratibu wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga akizungumza katika kikao hicho ambapo amewataka wenyeviti wa vitongoji kata ya Usanda na waelimishaji rika, kuwa elimu ambayo wameipata ya kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto wakaitumie vizuri kuisambaza kwa wananchi ili kuibadilisha na kuachana na vitendo hivyo vya ukatili likiwamo na suala la kuozesha watoto wa kike ndo za utotoni. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
 Mratibu wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga,amewataka wenyeviti wa vitongoji Kata hiyo ya Usanda na waelimishaji Rika, pia wakatoe elimu kwa jamii namna ya kuvunja ukimya na kuzungumza na watoto wao hasa wa kike kuacha mapenzi wakiwa katika umri mdogo pamoja na kuwa elezea madhara yake.
 Mtendaji wa Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Emmanuel Maduhu, akiwataka wenyeviti wa vitongoji kwenye Kata hiyo, kuitumie kikamilifu elimu ambayo wameipata kutoka Shirika hilo la Agape kutokomeza kabisa matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto likiwamo na suala la mimba na ndoa za utotoni, na ikibidi hata watumie sheria za kimili kwa kuwatenga wale ambao ni wagumu kubadilika.


 Wenyeviti wa vitongoji, waelimishaji rika, wazee maarufu na wa kimila wakisikiliza elimu ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto pamoja na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwenye kata hiyo ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

 Wazee maarufu na wa kimila katika kata ya Usanda wakiwa kwenye kikao cha shirika la Agape cha kuwajengea uwezo namna ya kupambana kutokomeza matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto pamoja na tatizo la mimba na ndoa za utotoni.
 Afisa elimu wa kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sospeter Kasonta, akilipongeza Shrika la Agape kwa kazi nzuri ambayo limeifanya kwenye kata hiyo, ambapo wameleta mabadiliko makubwa sana kwenye sekta ya elimu kwa kuongeza ufaulu hasa kwa wanafunzi wa kike.
 Afisa elimu wa Kata ya Usanda halmshauri ya wilaya ya Shinyanga Sospeter Kasonta, akiwataka wenyeviti wa vitongoji kwenye kata hiyo wakayaendeleze yale ambayo yalianzishwa na Shirika hilo la Agape, ikiwemo kutokomeza utoro wa reja reja kwa wanafunzi kwa kuwafuatilia hadi kwenye kaya zao wale wanafunzi ambao wanaonekana mitaani na kutokwenda shule.
 Afisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Elizabeth Mweyo, akitoa elimu ya ukatili kwa wenyeviti hao wa vitongoji na madhara yake, na kuwataka wakaitumie vizuri ndani ya jamii katika kuleta matokeo chanya na hatimaye kutokomeza vitendo hivyo hasa kwa wanawake na watoto ambao waathirika wakubwa.

 Wenyeviti wa vitongoji, waelimishaji Rika, wazee maarufu na wakimila  wakiendelea kusikiliza elimu ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto pamoja na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwenye kata ya Usanda
halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
 Elimu ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto  ikiendelea kusikilizwa.
  Elimu ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto  ikiendelea kusikilizwa.
  Elimu ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto ikiendelea kusikilizwa.
 Wenyeviti wa vitongoji, waelimishaji rika, wazee maarufu na wa kimila  wakiendelea kusikiliza elimu ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto pamoja na  kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwenye kata hiyo ya Usanda  halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
 Elimu ya ukatili ikiendelea kusikilizwa.
 Washiriki wa kikao hicho cha kupinga ukatili kwa wanawake na watoto kwenye kata ya Usanda wakichukua kumbukumbu za kwenda kuzitumia katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya kutomoeza ukatili huo likiwamo na suala la mimba na ndoa za utotoni.
 Wenyeviti wa vitongoji, waelimishaji Rika, wazee maarufu na wa kimila  wakiendelea kusikiliza elimu ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto pamoja na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwenye kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
 Mwenyekiti wa Kitongoji cha Uswahilini kata ya Usanda Daudi Shija, akielezea namna Shirika hilo la Agape lilivyosaidia kuibadilisha jamii katika kupunguza masuala ya ukatili kwa wanawake na watoto na kuahidi kuendeleza gurudumu hilo ikiwa elimu ambayo amepatiwa itamsaidia sana kuendeleza mapambano hayo ya kupinga ukatili.
 Mwenyekiti wa Kitongoji cha Butwale Paulo John, akielezea namna Shirika hilo la Agape lilivyosaidia kupunguza matukio ya ukatili ndani ya jamii likiwamo na suala la utekelezaji wa watoto ambapo sasa hivi wazazi wanaishi na watoto wao pamoja na kuwapeleka shule, wakiwamo na watoto walemavu ambao walifichwa lakini kwa sasa wapo shule.
 Mwenyekiti wa kitongoji cha Mwagala kata ya Usanda Ramadhani Kulwa,akielezea namna walivyo saidiwa na shirika hilo la Agape kupatiwa elimu ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto ambapo wao kama viongozi walishapiga marufuku watoto wa kike kwenda kucheza shoo kwenye harusi, ili kuwaepusha na vishawishi vya kutongozwa na kuambulia ujauzito.
 Mwenyekiti wa kitongoji cha Manyada kata ya Usanda John Masanja naye akitoa ushuhuda namna shirika hilo la Agape lilivyosaidia kupunguza matukio ya ukatili, ambapo na wao wamekuwa wakifuata nyayo hizo na kufanikiwa kutatua baadhi ya matukio hayo ya ukatili ndani ya jamii.
Awali katikakati ya kikao washiriki wakinyoosha mikono ya utayari wa kuendeleza mapambano ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ndani ya jamii.
Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post