Picha : AGAPE YAENDESHA BONANZA LA MICHEZO KUTOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UJINSIA KIJIJINI

Shirika lisilo la kiserikali AGAPE AIDS CONTROL PROGRAM la Mkoani Shinyanga linalojishughulisha na masuala ya jamii, limetoa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa njia ya bonanza la michezo kwenye vitongoji vya Buchamike,Shabuluba, Mwagala na Uswahilini vilivyopo pembezoni mwa kata ya Usanda Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.


Bonanza hilo limeendeshwa Ijumaa Mei 10, 2019 kwenye viwanja vya michezo vya kitongoji cha Buchambi kata ya Usanda ambapo kumefanyika michezo mbalimbali ikiwemo kukimbiza kuku, mbio za baiskeli pamoja na mpira wa miguu na washindi wamezawadiwa zawadi mbalimbali ikiwamo kupewa kuku pamoja na mbuzi.

Akizungumza kwenye bonanza hilo Mratibu wa mradi  wa afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika hilo la Agape Lucy Maganga, amesema wameamua kutoa elimu hiyo kwa njia ya michezo ili kufikisha elimu kwa wananchi, kuachana na masuala kupenda kuozesha wanafunzi ndoa za utotoni, pamoja na kuwapatia ujauzito na hatimaye kuacha masomo yao.

Alisema Shirika hilo limekuwa likiendesha mradi huo wa afya ya uzazi na ujinsia kwenye kata hiyo tangu mwaka 2017, kwa ufadhili wa shirika la Sida la nchini Sweden ambao unatarajiwa kuisha mwezi Juni 2019, lakini walikuwa hawafikii wananchi walio pembezoni kutokana na changamoto ya miundo mbinu ya barabara, lakini kwa sasa wameamua kufika hadi maeneo hayo ili elimu hiyo iweze kusambaa maeneo yote.

“Tumeendesha bonanza hili la michezo kwenye vitongoji ambavyo vipo pembezoni mwaka kata ya Usanda ili kutoa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa rika zote, ambayo itabadilisha mitazamo ya wananchi na kuachana na masuala ya kutongoza wanafunzi pamoja na kuwaozesha ndoa za utotoni ili waweze kutimiza malengo yao,”amesema Maganga.

“Pia tumewataka wananchi kuachana na masuala ya kufanya ngono zembe, ambayo yataweza kuwasababishia kupata magonjwa mbalimbali, na hatimaye kubakia kujiuguza na kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo na kushindwa kuinuka kiuchumi,”ameongeza.

Naye Kaimu mtendaji wa kata hiyo ya usanda Ester Pembelada,ametoa shukrani kwa shirika hilo la AGAPE kwa kutoa elimu hiyo ya afya ya uzazi na ujinsia, ambayo imekuwa na msaada mkubwa katika kupunguza tatizo la mimba na ndoa za utotoni tofauti na hapo awali.

Amesema amefarijika  shirika hilo kufika kutoa elimu hiyo ya afya ya uzazi na ujinsia hadi kwa wananchi ambao wapo pembezoni,kwani wengi wao elimu kama hizo huwa wanazikosa mahali ambapo ndipo kwenye matatizo makubwa ya wanafunzi wengi kukatishwa ndoto zao.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria bonanza hilo akiwemo Edward Ngassa na Lidya Jeremia, wameipongeza AGAPE kwa elimu hiyo ya afya ya uzazi na ujinsia na kubainisha kuwa itawasaidia kutambua umuhimu wa kusomesha watoto hasa wa kike pamoja na kulinda afya zao kwa kutopatwa na magonjwa.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Mratibu wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga akisalimia na wananchi wa vitongoji viliyopo pembezoni mwa kata ya Usanda kabla ya kutoa elimu hiyo ya afya ya uzazi na ujinsia kwa rika zote. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Mratibu wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia Lucy Maganga akitoa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa wananchi wa vitongoji vya kata ya usanda ambavyo ni Buchamike,Shabuluba, Mwagala, pamoja na Uswahilini, ili kuachana na masuala ya kutongoza wanafunzi na kuwaozesha ndoa za utotoni pamoja na kuacha ngono zembe ili kutopatwa na magonjwa.

Kaimu mtendaji wa kata ya usanda Ester Pembelada, akionya wanaume kuendekeza masuala ya michepuko, pamoja na kupenda kuozesha wanafunzi kwa tamaa ya kutaka kupata mifugo.

Wananchi wakisikiliza elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape.

Wananchi wakiendelea kusikiliza elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka shirika la Agape na kutakiwa kuacha tabia ya kuozesha wanafunzi ndoa za utotoni na kuwapatia ujauzito na kuzima ndoto zao.

Wananchi wakiendelea kusikiliza elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape kwa ufadhili wa shirika la Sida la nchini Sweden.

Wananchi wakiendelea kusikiliza elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape kwa ufadhili wa shirika la Sida la nchini Sweden.

Awali mashindano ya baiskeli yakianza kabla ya kutolewa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape, ambapo aliyeibuka mshindi ni Jumanne Dotto.

Mashindano ya baiskeli yakiendelea kwa wanaume ambapo mshindi wa kwanza amepewa zawadi ya mbuzi.

Mashindano ya baiskeli yakiendelea kwa wanawake ambapo mshindi aliyepatikana ni Lyidia Jeremia na alipewa zawadi ya mbuzi.

Mashindano ya kufukuza kuku yakiendelea ambapo Milembe Mabula aliibuka mshindi na kuondoka na kuku wake.

Timu ya kitongoji cha Shabuluba wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuanza mchezo wao wa fainali kwenye bonanza la elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape.

Timu ya kitongoji cha Buchamike wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa fainali na timu ya Shabuluba kwenye Bonanza hilo ambapo waliibuka washindi kwa kupiga mikwaju ya Penati na kupata magoli manne kwa mawili.

Mchezo wa mpira wa miguu ukichezwa kwenye bonanza hilo kwa fainali ya timu ya kitongoji cha Buchamike wenye jezi nyeupe pamoja na Shabuluba wenye jezi ya kijana ambapo hadi dakika 90 zinamalizika walitoka sare ya kufungana bao moja kwa moja.

Wananchi wakiendelea kutazama soka.

Mchezaji wa timu ya Buchamike akiwa ameumia kwenye bonanza hilo.

Wananchi wakiendelea kuangalia soka.

Mchezaji wa timu ya Shabuluba akipiga penati na kupata goli.

Wananchi wakiendelea kuangalia upigaji wa penati mara baada ya timu hizo za Shabuluba na Buchamike kutoka sare ya kufungana bao moja kwa moja.

Wananchi wakishuhudia upigaji Penati ili kupata ushindi.


Mchezaji wa timu ya Buchamike akifunga penati na kupata goli la, ambapo waliibuka na ushindi wa kupata Penati 4-2.

Wananchi wa kijiji cha Buchamike wakisheherekea ushindi.

Burudani zikiendelea kutawala kwenye bonanza hilo.

Mgeni rasmi kwenye bonanza hilo,Kaimu mtendaji wa Kata ya usanda Ester Pembelada mkono wa kulia akitoa zawadi ya kuku kwa mshindi Milembe Mabula. Kushoto ni mratibu wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga.

Kaimu mtendaji wa Kata ya Usanda Ester Pembelada (kulia) akitoa zawadi ya kuku kwa mshindi wa pili wa mbio za baiskeli kwa wanawake Juke Mashema, ambapo mkono wa kushoto ni mratibu wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga.

Kaimu mtendaji wa kata ya Usanda Ester Pembelada akitoa zawadi ya Mbuzi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli Lyidia Jeremia.Kushoto ni mratibu wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga.

Kaimu mtendaji wa Kata ya usanda Ester Pembelada mkono wa kulia akitoa zawadi ya mbuzi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli Jumanne Dotto.Kushoto ni mratibu wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga.

Kaimu mtendaji wa Kata ya usanda Ester Pembelada akikabidhi zawadi ya mbuzi kwa washindi wa pili wa timu ya mpira wa miguu ya Shabuluba.

Kaimu mtendaji wa kata ya Usanda Ester Pembelada akikabidhi  zawadi ya Mbuzi wawili kwa mshindi wa kwanza wa mpira wa miguu kutoka imu ya Buchamike, .Kushoto ni mratibu wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga.

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post