DIAMOND AELEZA SABABU ZA KUTOHUDUMIA WATOTO ALIOZAA NA ZARI

Msanii Diamond Platnumz ameeleza kile kinachoendelea kati yake na mzazi mwenzie Zari The Bosslady kuhusu watoto wao.

Muimbaji huyo kwenye kipindi cha Block 89 kupitia Wasafi FM amesema Zari amekuwa akizuia pindi anataka kuwaona watoto wake.

Amesema kila mwezi alikuwa akitoa dola za Marekani 2,000 ambazo ni wastani wa Sh5 milioni kwa ajili ya matunzo ya watoto. 

“Niseme ukweli kabisa, nina kama miezi mitatu hivi sijapeleka fedha za matunzo ya watoto kwa sababu mwenzangu hataki hata niongee na watoto, hebu fikiria hata kupitia mfanyakazi wa ndani amegoma nisiongee nao.

“Nilijaribu kuwasiliana na mtoto wake wa kiume, yule mkubwa lakini mwenzangu ameniwekea ngumu,” amesema.

Jitihada nyingine anazosema mwenzake amekuwa akizizima ni za kuwaleta watoto nchini akisema amemuwekea masharti kuwa lazima aje nao.

“Zari anataka aje na watoto, mimi nimemwambia mama nina mahusiano mengine nikamshauri mama yangu mzazi awafuate watoto lakini akakataa akasema labda niende kuwaangalia Sauzi (Afrika Kusini),” amesema.

Ameendelea kueleza kuwa, "Kuna kipindi Tiffah alizidisha muda wa kukaa South kwasababu anapassport ya Tanzania, ningekuwa nataka matatizo ningeweza kupiga simu mtoto akarudishwa Tanzania".

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post