HATIMAYE DIAMOND AFUNGUKA SABABU YA KUACHANA NA ZARI

Msanii Diamond Platnumz ameeleza kile kilichotokea kati yake na mzazi mwenzie Zari The Bosslady hadi kuachana kwao.

Muimbaji huyo kwenye kipindi cha Block 89 kupitia Wasafi FM amesema kuwa Zari alikuwa akimsaliti.

"Namheshimu Zari ni mzazi mwenzangu, alikuwa wife material, alikuwa anatoka na Peter wa Psquare, niliwahi kukuta sms nikamuuliza. Alikuwa anachepuka pia na Trainer wake na alikua anamleta hadi kwangu, lakini sijawahi kufunguka"

Ameendelea kwa kueleza kuwa, "Na ukweli sijawahi kuachwa na Mwanamke, Ukizingua nitakupiga matukio utaondoka mwenyewe".

“Mpaka nyumbani kwangu na mpaka picha pia ninazo ila mimi sio mtu wa kujifanya, mimi siongei mpaka naulizwa kwa nini sizungumzi, na kiukweli licha ya mambo yote hayo labda mimi nilikuwa ni chanzo kwa sababu mimi nilikuwa mwendawazimu kwelikweli na yeye alikuwa ananipenda sana ila mimi nilikuwa nampenda lakini sio kama yeye alivyokuwa ananipenda mimi”.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527