ZARI APANGUA TUHUMA ZA DIAMOND ' USINICHAFULIE MAISHA BRO...NIHESHIMU TAFADHALI' | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, April 24, 2019

ZARI APANGUA TUHUMA ZA DIAMOND ' USINICHAFULIE MAISHA BRO...NIHESHIMU TAFADHALI'

  Malunde       Wednesday, April 24, 2019
Mzazi mwenza wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Zari the Boss Lady, amefunguka baada ya msanii Diamond kuongea mengi kuhusu mahusiano yao yaliyopita ndani ya kituo chake cha redio cha Wasafi FM jana, April 23, 2019.

Diamond alifunguka mambo mengi ikiwemo Zari kumsaliti kwenye mahusiano, kuhusiana na kutoa sapoti kwa wanaye, na mambo mengine yaliyokuwa yanawahusu walipokuwa kwenye mahusiano.

Zari amejibu kwa kusema; “Sasa yale magoti mpaka Sauzi yalikuwa ya nini? Kule kuomba msamaha kwote kwa radio kwa nini? Kwani umekuwa comedian sasa? Usinichafulie maisha bro. Yameisha zamani kubali tu. Kiki zimekuwa ngumu mjini. Niheshimu tafadhali nakulelea watoto tena vizuri.

"Mimi sijawahi kuchepuka wakati nipo naye na ninajiapiza kama nimewahi kufanya hivyo basi lolote liwatokee watoto wangu.

“Sasa kama mtu amewahi kuikana damu yake kuna uongo gani mwingine anaweza kuacha kusema? Ni vyema kukiri makosa yako na kuyatumia kukua, bado unayo nafasi,” Amesema Zari

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post