WAZIRI UMMY AZINDUA BODI YA URATIBU YA ASASI ZA KIRAIA -NGO’S

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Waziri Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mh Ummy Mwalimu amezindua  Bodi ya  uratibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali  katika ukumbi wa Ofisi  ya Taifa ya Takwimu (NBS) Jijini Dodoma.

Akizungumza jijini Hapa waziri Ummy amesema kuwa  Bodi ina jukumu la kutoa miongozo ya kisera pamoja na kuchunguza na kuhoji ili kuhakikisha uzingatiaji wa katiba za mashirika yasiyo ya kiserikali.

Aidha, Waziri ummy ameongeza kuwa ni wajibu wa bodi  hiyo kujielekeza  katika kuhakikisha sekta hiyo inajiendesha kwa misingi ya uwazi na uwajibikaji ndani ya serikali , ndani ya mashirika yasiyo ya kiserikali na kwenye sekta binafsi.

Mbali na hilo waziri Ummy amesema bodi hiyo itafanya kazi kwa kuzingatia sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali lakini pia kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni zilizoko.

Rukia masasi ni mwenyekiti  Bodi ya mashirika yasiyo ya kiserikali aliyemaliza muda wake amesema kuwa  bodi  ni chombo muhimu kwasababu  inabeba  NGO’s na  ni mwakilishi wa  asasi za kiraia ,NGO’s na pia ni  mwakilishi wa serikali hivyo ni kama kiungo kwani  serikali na  asasi za kiraia,NGO’s  ni wadau wanaoshirikiana katika maendeleo .

Kwa upande wake katibu mkuu wizara ya afya maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto anayeshughulikia idara kuu ya maendeleo  ya jamii, Dkt John Jingu amesema  sekta ya mashirika yasiyo ya kiserikali ni sekta ambayo inamchanganyiko wa kipekee kwani ni sekta kubwa na nipana.

Naye Mwenyekiti Mpya wa Bodi hiyo  Richard  Sambaiga amesema jukumu lao kubwa ni kuwezesha uratibu na utendaji kazi wa sekta hiyo ili uweze kustawi kwa maslahi ya umma wa Tanzania.

Hatahivyo, Waziri ummy amesema  asasi za kiraia ,NGO’s  ni sekta kubwa na nimuhimu katika kujenga na kushiriki  katika Maendeleo ya kiuchumi,kisiasa ,kijamii na kiutamaduni.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post