SRI LANKA YATANGAZA HALI YA DHARURA, IDADI YA WALIOUAWA YAFIKA 290


Rais wa Sri Lanka Maithripala Sirisena ametangaza hali ya dharura kuanzia saa sita usiku Jumatatu kufuatia shambulizi la kigaidi kwenye makanisa na hoteli za kifahari siku ya Pasaka. Idadi ya waliouawa yafika 290.

Taarifa ya Kitengo cha habari cha serikali ya Sri Lanka imesema, ''Serikali imeamua kutangaza sheria inayolenga kuzuia ugaidi ambayo itaanza kuheshimiwa saa sita usiku leo.''


 Taarifa hiyo imefafanua kuwa hatua hiyo itahusiana tu na shughuli za kuzuia ugaidi, na haitaingilia uhuru wa watu wa kutoa mawazo yao.

Msemaji wa serikali mjini Colombo Rajitha Senaratne amesema kuwa serikali ya Sri Lanka inaamini kuwa kundi lenye itikadi kali la nchini humo lijulikanalo kama NTJ (Nationa Thowheeth Jama'ath) ndilo limefanya shambulizi hilo, na ameongeza kuwa uchunguzi ulikuwa ukifanyika kuangalia iwapo kundi hilo lilipata usaidizi kutoka nje ya nchi.

Tayari watu 24 wamekamatwa kuhusiana na shambulizi hilo huku Marekani ikionya kuhusu uwezekano wa mashambulizi mengine ya kigaidi katika tahadhari waliyoitoa kwa wasafiri wanaokwenda Sri Lanka.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post