SPIKA NDUGAI ATAKA WALIMU WA SAYANSI WAPEWE KIPAUMBELE WAKATI WA KUTOA AJIRA

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Spika wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai ameishauri Serikali  kuwa na mpango wa kutoa kipaumbele cha kwanza katika kuajiri walimu wa  Masomo ya Sayansi  ili kupunguza uhaba wa walimu hao hapa nchini.

 
Mhe.Ndugai ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akitoa mchango wa nyongeza  baada ya Mbunge wa Buhigwe Mhe.Albert Obama aliyehoji mpango wa Serikali kuongeza walimu wa Masomo ya Sayansi.

Mhe.Ndugai katika Msisitizo wake amesema kuna baadhi ya shule katika jimbo lake  unakuta kuna mwalimu mmoja tu wa Masomo ya Sayansi hususan somo la hesabu hivyo kuna haja ya serikali katika awamu nyingine ya ajira ikaajiri walimu pekee wa Masomo ya Sayansi hata kama ni elfu nne huku Mbunge wa Buhigwe Alrbert Obama  Ntabaliba akihoji pia juu ya kuongeza vifaa vya Maabara.

Akijibu Maswali hayo,Naibu Waziri wa  nchi,Ofisi ya Rais na Serikali za Mitaa Mwita Waitara amesema serikali inafanya mchakato wa kuajiri zaidi ya walimu elfu nne kwa kuzingatia maeneo yenye upungufu zaidi na awamu ya pili  ya kutoa ajira serikali itazingatia maeneo yenye mapungufu zaidi  walimu wa Masomo ya Sayansi.

Hata hivyo Naibu Waziri,Waitara amesema kwa mwaka wa fedha 2018/2019  serikali inatarajia kununua na kusambaza vifaa  vya Maabara katika  shule za sekondari 1250 zilizokamilisha vyumba vya maabara hapa nchini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527