SPIKA NDUGAI AMVAA TENA CAG PROF. ASSAD.....ANAMPA WAKATI MGUMU SANA RAIS | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, April 14, 2019

SPIKA NDUGAI AMVAA TENA CAG PROF. ASSAD.....ANAMPA WAKATI MGUMU SANA RAIS

  Malunde       Sunday, April 14, 2019
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kitendo cha Mdhibiti Mkuu na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad kuendelea kuwepo ofisini mpaka sasa ni kumpa rais wakati mgumu kwa kuwa wao bunge wameshaeleza kuwa hawamtaki.
Ndugai ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dodoma ambapo amesema kwamba kwa kitendo cha Bunge kumkataa Prof Assad alipaswa ajiongeze kwa kujiuzulu.

"Tunataka tumuoneshe Prof. Assad kuwa Bunge halichezewi, simuelekezi kazi  ila anatakiwa ajiongeze kama ni kujiuzulu au la! maana tushamwambia  hatumtaki, anavyoendelea kubaki ofisini ni kumpa tu wakati mgumu Rais. "Sisi kama Bunge hatutaki hilo neno dhaifu, kwa sababu Bunge kama Bunge  halifanyiwi tathmini na ofisi ya CAG ila wanaofanyiwa tathmini ni  watendaji wa Ofisi hiyo hivyo hawakupaswa kudhihakiwa na lugha hiyo  inayotajwa kuwa ya kihasibu".

Aidha kuonyeshwa kukerwa na neno 'Dhaifu analoendelea kulitumia Prof Assad, Ndugai amesema kwamba  kama yeye analipenda sana neno hilo ajiite na kwamba wao kama bunge wameikataa na hawalipendi.

Kuhusu kazi za CAG, Spika amefafanua kwamba; "Hatuna tatizo na ripoti ya CAG…tatizo letu ni maneno ambayo Prof. Assad ameyatoa akiwa Marekani, na alipoita waandishi akarudia  tena, maneno yale sie tumeyakataa sio ya kistaarabu.Spika Ndugai amemsifu Profesa Assad kwa ujasiri wake huku akiufananisha na ujasiri wa mbwa kumtukana mtu anayemlisha.

"Unatukana hadi mkono unaokulisha, inahitaji ujasiri na jamaa ana ujasiri. Ila ni ujasiri ule wa mbwa anayemtukana anayemlisha," amesema.

Hata hivyo, Ndugai amesema hana chuki binafsi na Assad bali tatizo ni lugha tu aliyotumia ya kuliita Bunge dhaifu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post