SPIKA NDUGAI AKABIDHIWA WITO WA WANANCHI 15,000 WALIOPINGA BUNGE KUTOFANYA KAZI NA CAG

Wakati kampeni ya mtandaoni kupinga azimio la Bunge la kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad  ikifikisha zaidi ya watu 15,000, waraka wa kampeni hiyo umefikishwa katika ofisi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai

Waandaaji wa kampeni hiyo ambao ni Taasisi ya Change Tanzania wamesema leo Jumatatu Aprili 8, 2019 kuwa maoni hayo yaliyokusanywa yamefikishwa ofisi ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam na mengine yakitarajiwa kutumwa jijini Dodoma kuanzia kesho Jumanne.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527