KAGERA SUGAR WAITANDIKA SIMBA SC 2 -1Timu ya Simba imekubali kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Mabao mawili ya haraka waliyopata Kagera Sugar yaliwachanganya zaidi Simba na kukubali kwenda mapumziko wakiwa nyuma. 

Katika mchezo huo ambao Simba ilikwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa mabao 2-0 ikiwa nimra aya kwanza tangu msimu huu uanze, watajilaumu wenyewe kutokana na jinsi walivyocheza chini ya kiwango na kuwapa nafasi wapinzani kutawala mpira. 

Kagera Sugar walianza kulisakama lango dakika za mapema kupitia kwa Nahodha wao Msaidizi, Paulo Ngalyoma licha ya kutofunga,ambapo dakika ya 17 Kasim Hamis kuipatia bao la kuongoza akimalizia kazi nzuri ya Venance Ludovic kutokana na mabeki kushindwa kuzuia vyema lango. 

Hata hivyo Kagera Sugar waliendelea kutakata kwa mashambulizi yao na dakika ya 42 Ramadhan Kapera akawainua mashabiki wao ambao wamebebelea miwa kwa kufunga bao la pili kwa kichwa akiunganisha krosi Ally Ramadhan. 

Hata hivyo Emmanuel Okwi aliifungia Simba bao la kwanza dakika ya 62, jambo lililowarudisha mchezo wachezaji wa tiu hiyo.

Simba ilijaribu kupambana lakini ilionekana wazi kulemewa na kashkashi ya wapinzani na kusababisha mashabiki wake kupooza jukwaani.
Via >> Mwanaspoti

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post