SHOGA AOKOKA, SASA NI 'MUINJILISTI' ANACHAPA INJILI BALAA

Jamaa mmoja anayetambulika kuwa shoga nchini Ghana amesisimua mitandao ya kijamii baada ya kuamua kubadilisha mwenendo yake na kuokoka.

Aaron Akrong alianza kwa kunyoa nywele zake ambazo alikuwa ameziweka mchano wa aina ya Dreadlocks na pia kubadilisha mtindo wake wa kimavazi punde alipookoka.

Akrong ambaye alikuwa akivalia mapambo ya kike ikiwemo hereni na vipuli kwa sasa hayavai kulingana na picha ambazo amekuwa akichapisha mitandaoni.

 Kupitia mitandao ya kijamii, Akrong amekuwa akieneza injili kupitia video kadhaa akihubiri neno la bwana. 

Aidha, wainjilisti wenzake walimpongeza kwa hatua hiyo na kumtaka aendelee kueneza injili.

 "Jamaa huyu Akrong ni sababu moja ya kunifanya mimi nizungumzie ukuu wa Mungu kila wakati, Akrong amekuwa shoga kwa zaidi ya miaka 20 na amekuwa akitumia dawa za kulevya, hata amekuwa akitaka ushoga uhalalishwe nchini Ghana hadi Mungu alipomuokoa, kwa sasa ni muinjilisti," Pasta mmoja alisema.

 Haya yanajiri siku chache tu baada ya mhubiri mwingine wa kike Jacinta Nzilani kujitokeza wazi na kusema anajivunia kuwa msagaji na kuwa anajutia kuolewa kwa miaka 25. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post