RAIS WA SUDAN OMAR AL-BASHIR ANG'OKA MADARAKANI


Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Reuters, Rais wa Sudan Omar Al-Bashir  tayari ameshaachia ngazi na makubaliano juu ya kuundwa kwa serikali mpya yanafanyika. 

Baadhi ya viongozi wa juu wa serikali akiwemo Waziri wa zamani wa ulinzi na kiongozi wa juu wa chama tawala wanashikiliwa na jeshi. 


Tangu asubuhi ya leo,  wanajeshi walikuwa wametanda katika makazi rasmi ya rais  Omar Al-Bashir na kuzingira njia zote muhimu za kuingia na kutoka mji mkuu wa Khartoum na  uwanja wa ndege  Khartoum umefungwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527