RADI YAVUNJA NYUMBA KISHA KUUA WATU WATANO WA FAMILIA MOJA TABORA

Na Editha Edward-Tabora 

Watu Watano wa Familia moja katika kijiji cha Isonge Kata ya Sikonge Mkoani Tabora wamefariki dunia na watatu kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na mvua na upepo mkali. 

Tukio hilo lililoibua simazi kubwa limetokea usiku wa saa tano kuamkia leo katika kijiji hicho.

 Kaimu Mganga Mfawidhi Wilaya ya Sikonge Mathew Sipemba amesema alipata taarifa hiyo kutoka polisi juu ya tukio hilo na kukuta watu Watano walikuwa tayari wamepoteza maisha

"Ajali ya radi sio nzuri ni kama moto watu hawa wamejikuta wanavuta hewa ya harufu kali na kuunguza mapafu jambo ambalo limepelekea kupoteza maisha kwa watu hawa",amesema Sipemba.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Kamishina msaidizi Emmanuel Nley amesema radi hiyo ilisababisha ukuta wa nyumba waliyokuwa wamelala familia hiyo kupasuka na kusababisha vifo hivyo.

"Nyumba Ilikuwa imejengwa kwa udongo na makuti na kuezekwa kwa nyasi mvua iliponyesha ilisababisha ukuta kupasuka na kupelekea tukio hilo kutokea",amesema Nley

Kamanda Nley amesema katika tukio hilo waliopoteza maisha ni Mhindi Peter, Vailleth Juma, Gress Juma Kulwa Lukanya na Nyanzobe Juma

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Peter Nzalalila amesema tukio hilo likmeibua simanzi kubwa na amewataka Wananchi wa eneo hilo kuacha kuhusisha tukio hilo na imani za kishirikina.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post