MAROBOTA YA PAMBA YAUA WANAFUNZI WAWILI

Wanafunzi wawili wa familia moja, Daniel Mnyema (9) na mdogo wake Mateo Jacob (7) wamekufa baada ya kufunikwa na marobota ya tumbaku yaliyowaporomokea ndani ya chumba walichokuwa wamelala ambacho kiligeuzwa kuwa stoo ya kuhifadhia zao hilo.

Watoto hao walikuwa wakisoma katika shule shikizi ya Kambanga iliyopo katika kitongoji cha Kambanga kijiji cha Igalula, wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi.

 Ofisa wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa masharti ya kutoandikwa majina yake gazetini kwa sababu sio msemaji wa jeshi hilo, alikiri kutokea kwa vifo vya watoto hao wawili huku akisisitiza kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Akisimulia mkasa huo kwa undani, Mwenyekiti wa kijiji cha Igalula, Yasin Mohamed alisema kuwa vifo vya watoto hao ambao walikuwa wakiishi na wazazi wao katika kitongoji cha Kambanga, vilitokea juzi usiku wakiwa wamelala katika chumba ambacho kiligeuzwa stoo ya kuhifadhiwa tumbaku. 

Akifafanua alisema kuwa siku hiyo ya tukio wazazi wa watoto hao walishinda shambani hadi jioni ambapo walirudi nyumbani wakiwa wamechoka hivyo walilazimika kulala mapema baada ya kula chakula cha jioni.

“Kabla ya wazazi hao kwenda kulala waliagana na watoto ambao nao waliingia na kulala kwenye chumba chao ambacho tayari kilikuwa kimegeuzwa stoo ya kuhifadhia tumbaku ambayo ilikuwa tayari imekaushwa na kufungwa kwenye marobota ikisubiri kuuzwa wakati wa msimu wa ununuzi wa zao hilo utakapowadia, “ alieleza.

Aliongeza kuwa wakati watoto hao wakiwa wamelala kwenye chumba hicho, marobota ya tumbaku yaliwaangukia na kuwafunika na kuwasababishia umauti. “Kulipopambazuka mama wa watoto hao alishtuka kuona mlango wa chumba walimokuwa wamelala watoto wake kikiwa bado kimefungwa kwa kuwa haikuwa kawaida ya watoto hao kuchelewa kuamka,” alisema.

Alisema alipojaribu kusukuma mlango haukufunguka ikamlazimu kuomba msaada kwa majirani ambao walivunja dirisha la chumba hicho ndipo walipogundua watoto hao wamefunikwa na marobota ya pamba. Mwenyekiti Mohamed alieleza kuwa pamoja na majirani hao kuyatoa marobota.

Chanzo - Habarileo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post