Utafiti : ULAJI NYAMA UNACHANGIA KIFO CHAKO MAPEMA KWA ASILIMIA 23



Na Hassan Daudi na Mitandao

Wakati kwa baadhi ikionekana ulaji wa nyama ya nguruwe ‘kitimoto’, ng’ombe na mbuzi kuwa ni ishara ya kipato kizuri, hata hivyo vitoweo hivyo vimetajwa kuwa miongoni mwa vyanzo vya vifo vya mapema, ikichangia kwa asilimia 23.

Utafiti huo mpya unakubaliana na ule uliowahi kufanywa na Taasisi ya Kansa nchini Marekani, ambao ulihoji watu 536,000 wenye umri wa miaka 50 hadi 71 waliojitaja kuwa ni walaji wa nyama nyekundu.

Majibu ya utafiti huo yalionesha kuwa asilimia 26 ya wale waliokuwa wakitumia nyama kwa kiasi kikubwa walikuwa wakisumbuliwa na magonjwa tisa sugu, ikiwamo saratani inayosababishwa na madini ya chuma aina ya Heme yanayopatikana katika nyama nyekundu.

Utafiti wa sasa uliofanywa hivi karibuni na Chuo Kikuu cha Eastern Finland na kuchapishwa na jarida la American Journal of Clinical Nutrition, nao umezidi kukazia mwelekeo ule ule.

Majibu yake yalitokana na watu 2,600 waliohojiwa juu ya mpangilio wao wa kula, wote wakiwa ni watumiaji wakubwa wa nyama nyekundu (ng’ombe, mbuzi n.k.) hapo ndipo watafiti walipobaini kwamba waliokuwa na kawaida ya kula gramu 200 za nyama kwa siku walikuwa hatarini zaidi, ukilinganisha na wenzao wa chini ya gramu 100.


Chanzo - Mtanzania

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527