NAIBU WAZIRI WA AFYA ATHIBITISHA KUWEPO KWA HOMA YA DENGUE TANZANIA


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile, amethibitisha kuwepo kwa homa ya dengue nchini ambapo watu 307 wamegundulika kuwa na ugonjwa huo katika mikoa ya Dar es salam na Tanga tangu Januari hadi sasa.

“Tatizo la homa ya dengue tunalo, kwa sasa tumeanza kubaini wagonjwa waliougua Dar es Salaam na Tanga, hatujapata vifo vyovyote .Mpaka sasa tunao wagonjwa takriban 307 Dar es Salaam  na Tanga lakini hakuna aliyeathirika, nashauri watoa huduma kuwapima wagonjwa iwapo watabainika wanaumwa wapewe tiba stahiki,” amesema Dk Ndugulile na kuongeza:

“Asilimia zaidi ya 70 ya homa tulizonazo si malaria, kuna UTI, homa ya matumbo haya yote yanasababishwa na virusi na dengue ni moja ya inayosababishwa na virusi, hatuwezi kukataa kwamba haupo upo ndani ya Tanzania tunachokifanya sasa ni kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji na kuwa na takwimu sahihi kwenye hospitali za umma na binafsi.”


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post