NABII WA KIUME AVAA CHUPI YA WANAWAKE AKIHUBIRI KANISANI


Nabii mmoja kutoka nchi ya Ghana amewaacha wengi vinywa wazi baada ya kuvalia nguo za wanawake wakati akiwahubiria waumini wake.


 Mchungaji huyo kwa jina Kofi Oduro aliyavalia mavazi hayo juu ya mavazi yake rasmi huku akizunguka kanisani humo wakati wa ibada.
Kulingana na video iliyosambaa Instagram, nabii huyo alikuwa anawafunza wanawake jinsi ya kunadhifisha ndoa yao na kuifanya iwe ya kufana wakiwa katika chumba cha kulala na wapenzi wao.

 Hivyo basi, katika hali ya kusisitiza kiini cha mafunzo yake, Kofi aliyavalia mavazi ya ndani ya wanawake ili kuhakikisha kuwa ujumbe wake umenakiliwa kisawasawa na wafuasi wake.

 Cha kushangaza ni kuwa, wanawake ambao walikuwa wamehudhuria kongamano hilo, waliketi kitako na kutulia huku wakimsikiza kwa makini. 

"Wanawake wengi hujisahau wakati wanapooloewa. Nawashauri enyi wanawake wote mlioolewa, ili kuifanya ndoa yako iwe ya kufana, sharti uwe mchangamfu," nabii huyo alisema. 

Baada ya kuzua kioja cha kuvaa chupi, alitwaa pajama ya wanawake na kuivalia wakati uo huo akiendelea na mafunzo kuhusu ndoa bila hata aibu. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post