MZEE WA KANISA ANASWA LIVE KWENYE SHAMBA LA MUUMINI AKIWA UCHI NA CHUPI ZA KIKE

Mzee mmoja wa Kanisa la Pentekoste la Kyethami Kaunti ya Kitui  nchini Kenya ambaye amekuwa akitumia ujanja wa kuwalaghai waumini hatimaye amekamatwa akiwa uchi wa mnyama katika shamba la mkazi mmoja. 
Mzee huyo aitwaye Kyalo Kavali, amefumaniwa katika boma la mmoja wa waumini akipandikiza vimbwanga ili kurejea baadaye, na kuiombea familia hiyo kabla ya kuwaonyesha kulipokuwa vitu hivyo ambavyo mara nyingi alidai, ndivyo vilivyokuwa vikiihangaisha familia hiyo. 

Miongoni mwa vitu alivyokamatwa navyo Kavali ni fuvu la kichwa, chupi za wanawake na nywele za binadamu na vifaa vingine alivyodai ni vya maombi. 

Inaelezwa kuwa Mzee huyo wa Kanisa huwa anawataka watu kumpa pesa kabla ya kuwaombea na alikuwa akiingia katika mashamba ya watu usiku na kupandikiza vimbwanga.

Wakazi waliokuwa na hasira na waliotaka kumuua walisema walikuwa na imani kubwa naye tangu awali, lakini hawakujua kumbe ni laghai. 

"Alikuja nyumbani kwangu na kuniambia alitaka kuniombea na ikiwa ningempa sadaka kidogo," alisema Jemima Muthemi.

Baada ya kupokea ‘sadaka', waumini walipokea maombi na kumiminiwa baraka tele kutoka kwa mzee huyo.

 "Huwa navizika vimbwanga katika maboma yao. Kisha mimi huvichimbua na kuwalipisha pesa, hivyo ndivyo ninavyotengeneza pesa," Kavali alisema.

 "Tunamwamini sana mzee huyu kwa kuwa ni mtu anayependa maombi sana," alisema Justus Kakoma, ambaye pia ni mzee wa kanisa hilo.

Mshukiwa huyo aliokolewa na chifu wa eneo hilo David Chumbo na kuruhusiwa kuvaa nguo zake kabla ya kupelekwa kituo cha polisi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527