MRITHI WA FATMA KARUME TLS AFUNGUKA BAADA YA USHINDI


Rais mpya wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika Dkt Rugemeleza Nshala amesema katika uongozi wake atahakikisha Mawakili atakaowaongoza anawapatia mafunzo na kuwawekea mazingira mazuri ya kufanya kazi.

Dkt Nshala ametoa kauli hiyo Arusha mara baada ya kushinda nafasi ya Urais wa chama hicho akipokea kijiti kutoka kwa Fatma Karume, ambaye amemaliza muda wake baada ya kukiongoza chama hicho kwa mwaka mmoja.

"Tutapigania sheria kwa nchi yetu, na tutawaendeleza wanachama wetu waweze kufanya kazi kwa uhuru bila kunyanyaswa kutishwa na kuwekwa ndani kama ilivyojitokeza hivi sasa, Mawakili ni watu muhimu kuhakikisha nchi yetu inatawaliwa kisheria" amesema Dkt Nshala

Dkt Rugemeleza Nshala ameshinda nafasi hiyo kwa kupata kura 629 kati ya wajumbe 1162 ambapo pia miongoni mwa miongoni mwa wajumbe ambao walichaguliwa kwenye nafasi ya Wajumbe wa Baraza la chama hicho ni Wakili Jebra Kambole.

Uchaguzi wa TLS umefanyika April 6, 2019 ambapo Rais aliyemaliza muda wake ni Fatma Karume ambaye alipokea kijiti kutoka kwa Mbunge Singida Mashariki Tundu Lissu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527