Mbunge wa CUF Maftaha Nachuma Ataka Polisi Wasitumike Kwenye Uchaguzi

Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftaha Nachuma (CUF) ameitaka serikali isiwatumie askari polisi wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika baadae mwaka huu.

Nachuma ameyasema hayo bungeni leo Aprili 11, alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya Tamisemi, Utumishi na Utawala bora kwa mwaka wa fedha 2018/19.

 Amesema kwamba pamoja na kwamba polisi wanatakiwa kulinda amani, serikali imekuwa ikiwatumia kuharibu uchaguzi na kukipendelea Chama cha Mapinduzi (CCM) na hicho ni kinyume na sheria ya utawala bora ambayo inatambua mfumo wa vyama vingi nchini.

Nachuma pia ameitaka tume ya uchaguzi iwe huru wakati wa chaguzi za serikali za mitaa ili kila chama kishiriki kwa mujibu wa sheria.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post