ASKARI POLISI AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI KAHAMA ..RPC ASEMA CHANZO NI KUTOZAAAskari aliyejiua kwa risasi
Askari polisi wa kituo cha Polisi wilaya ya Kahama H1363 PC Gideon Clement (30) mkazi wa Muleba mkoani Kagera
leo Alhamis Aprili 4,2019 majira ya saa moja nusu amejiua kwa kujipiga risasi shingoni na kutokea kichwani  wakati akiwa kwenye lindo katika  benki ya Access mjini Kahama.


Akizungumza na Malunde1 blog kwa simu,Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao amesema sababu za askari huyo kujiua ni kutokana na kutofanikiwa kupata mtoto licha ya kuishi kwenye ndoa  na mkewe kwa muda wa miaka mitano.

"Sababu za kujiua kwake ameeleza kwa ujumbe aliotuma kwa mke wake kwamba hana sababu za kuendelea kuishi kwa sababu hajajaliwa kupata mtoto na amekaa kwenye ndoa kwa muda wa miaka mitano na mke wake ambaye ni mwalimu na inasemekana jana alilalamikia sana jambo hilo na alianza kuonesha dalili kwa kumtumia mkewe ujumbe wa simu akieleza kuhusu mali zake vikiwemo viwanja viko wapi",ameeleza Kamanda Abwao.

Kamanda Abwao amesema taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Muleba kwa ajili ya mazishi zinaendelea.

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post