KUFANYA VIBAYA KWA SERENGETI BOYS, WAZIRI MWAKYEMBE AWALAUMU MAWAKALA


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amedai miongoni mwa sababu za timu ya Serengeti Boys kufanya vibaya ni baadhi ya Mawakala wa wachezaji wa nchi za nje kuwaahidi baadhi ya wachezaji kiasi kikubwa cha pesa na kutakiwa timu kubwa.

Mwakyembe alikuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia wakati wa mjadala wa Wizara hiyo aliyehoji kitendo cha Serengeti Boys kutofanya vizuri kwenye michuano ya AFCON chini ya miaka 17 kwa kuambuliwa kichapo katika mechi zote tatu walizocheza na kutupwa nje ya michuano.

Akihoji suala hilo Mbunge Mkamia amesema kuwa, "huwezi ukaandaa mashindano ukashika nafasi ya mwisho hata Korea aliishia robo fainali, nilishangazwa pale kamati ilipotangaza wakichukua ubingwa watawapa magari na milioni 20, ni sawa na mtoto wa miaka 8 ana birthday, unamwambia nitakununulia gari, hatukuiandaa timu vizuri hata mashindano waliofanya vizuri yalikuwa ni bonanza."

Akijibu hoja hiyo Waziri Mwakyembe amesema kuwa, "vijana wetu walikuwa na presha ya kuibeba Tanzania, pia nawalaumu Mawakala waliokuja  nchini wakina Diouf, Etoo waliwaambia watoto wadogo tunawahitaji kwenye timu yetu tutakulipa milioni 100, wakawa wanacheza kwa kuangalia zile hela. Baadhi ya  wazazi wakawaambia watoto wao wasicheze watavunjika mguu."


Msikilize gapo chini akiongeaDownload/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post