Mkazi wa Kijiji cha Nyantorotolo Kata ya Nyankumbu Halmashauri ya Mji wa Geita, Patrick Andrew (41) anashikiliwa na Polisi Mkoa wa Geita kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa kufikia wa miaka 7, ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema kwa sasa jina la mtoto huyo wanalihifadhi, lakini alikuwa akisoma Shule ya Msingi Nyankumbu, ambapo ameeleza mwanamume huyo alifanya kitendo hicho majira ya saa tano usiku siku ya mkesha wa Pasaka
Aidha Kamanda Mponjoli amesema mtu pekee ambaye aligundua mtoto kufanyiwa vitendo hivyo vya kinyama ni mama mzazi wa mtoto huyo, ambaye pia alibainisha kulihifadhi jina lake.