ANUSURIKA KUFA BAADA YA KUDUNGWA VISU MARA 17 NA MMEWE


 Mwanamke aitwaye Peninnah Wangechi mwenye umri wa miaka 30 anauguza majeraha mabaya aliyoyapata baada ya mume wake kumvamia na kumdunga visu mara 17  kisha kutoroka baada ya kuufanya unyama huo.


 Mama huyo wa watoto watatu alipata majeraha mgongoni, usoni na kifuani.

 Peninnah Wangeci ambaye amelazwa katika hospitali ya Kaunti ndogo ya Karatina alinusurika kifo baada ya kudungwa kisu mara kumi na saba kufuatia mgogoro wa kinyumbani.

Kwa mujibu wa Citizen Digital, kisa hicho kilitokea Jumanne, Aprili 9,2019 ambapo mumewe, Samuel Ndirangu alimtishia kabla ya kumtendea unyama huo na kisha kutoroka. 

Wangeci, alisema ndoa yake imekuwa ikikabiliwa na migogoro ya mara kwa mara na kwamba siku hiyo haikuwa ya kwanza kwa mumewe kumtishia.

Mkurugenzi wa hospitali hiyo Benson Ngari alisema, mgonjwa yupo katika hali nzuri ijapokuwa alipoteza damu nyingi.

Chanzo - Tuko

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post