POLISI KIGOMA WADAI KUUA MAJAMBAZI 24


Jeshi la Polisi Tanzania limeendesha Operesheni sehemu mbalimbali za nchi ili kupambana na wahalifu waliokuwa wanavamia majumani na kuteka magari njiani kwa kutumia silaha za moto.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Nchini  CP, Liberatus Sabas amesema operesheni hiyo iliyofanika katika Mkoa wa Kigoma imefanyika ndani ya miezi mitatu ambayo ilianza mwezi wa kwanza mpaka mwezi wa tatu mwaka huu na kufanikiwa kukamata silaha 14 aina ya SMG na risasi 350 pamoja na mafanikio hayo Jeshi la Polisi limefanikiwa kuua majambazi 24 katika majibizano ya kurushiana risasi na polisi ambapo katika mapambano hayo askari wawili walijeruhiwa na majambazi ila mpaka sasa wanaendelea na matibabu.

Aidha kamishna Sabas, amesema wahalifu hao wanaotoka nchi za jirani ambazo hazina utulivu wa kisiasa, huku akiwaonya wahalifu hao wanaotoka  nchini jirani kuwa wajue wataingia ila hawatatoka na wakae wakijua hakuna mwalifu atakaebaki salama pia akiwataka wale wanaoingia nchini kwa kutumia miamvuli ya wakimbizi na wao hawatakuwa salama kwani wakae wakijua Tanzania ni kisiwa cha amani.

Kamishna Sabas amewataka  wananchi kuendelea kutoa ushirikiano baina yao na Jeshi la Polisi ili kukabiliana na wahalifu wa ndani na wale wanaotoka nje ya nchi na kuwatumia salamu kuwa Tanzania si sehemu salama kwa wahalifu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post